Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo
madarakani.
Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na
wanachama.
Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni
kwenye mkutano huo.
Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi wa
sasa.
Mwanachama mwingine akimchana ‘live’ Aden Rage kuhusu sakata la Mbuyu
Twite na Kelvin Yondani.
Wanachama wakitoka kwa amani baada ya kumaliza
mkutano.
Askari wakiangalia suala la usalama.
WANACHAMA wa klabu ya
Simba, leo walifanya kikao cha dharura kwenye Hoteli ya Star Light Mnazi Mmoja
jijini Dar na kuung’oa uongozi wa klabu hiyo uliopo madarakani chini ya
Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage kufuatia mwenendo mbaya wa timu
yao.
Wanachama hao
wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,
Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha kiongozi aliyejiuzulu hivi
karibuni, Zacharia Hans Poppe. Wanachama hao wamesema wanatarajia kuitisha
mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu
inayoendelea ili kuepusha kuivuruga timu.
SOURCE:GLOBALPUBLISHER
Post a Comment