kusahihishiwa.Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa,
wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama matokeo
hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa, wanafunzi
waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000
na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya
habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi
waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka
huu na kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa,
NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza kufanya
kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini, kilichowashangaza walimu hao
ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye
aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza
hilo.
Wakizungumza na
NIPASHE, baadhi ya walimu walisema walioshiriki kusahihisha mitihani hiyo
walisema kuwa maoni yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu kwamba matokeo
mabaya ya mtihani huo yalitokana na uchakachuaji, hayakuwa ya kweli.Katibu
Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na NIPASHE jana
alithibitisha kuwa mitihani ya wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa
Machi 12 mwaka huu.
Dk Ndalichako
alisema hata hivyo, hana taarifa kama matokeo ya wanafunzi hao yanaonyesha kuwa
wanafunzi wengi wamefeli zaidi kwa kuwa alikuwa safarini kikazi.“Unavyozungumza
na mimi nipo Arusha na wageni, sifahamu kama baada ya kusahihishwa upya mtihani
wa wanafunzi waliokata rufaa matokeo yamekuwaje, nitafahamu baada ya kurejea Dar
es Salaam Jumatano wiki hii,” alisema Dk Ndalichako ambaye hata hivyo, hakutaja
idadi ya wanafunzi waliokata rufani.Dk Ndalichako alisema suala la kufeli zaidi
wanafunzi waliokata rufaa linawezekana kutokea kwa sababu kila mwaka imekuwa
ikijitokeza hali kama hiyo, hivyo ni jambo la kawaida
NIPASHE
Post a Comment