Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA BARABARA ILI ZIDUMU KIPINDI KIREFU



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Ruvuma leo katika ukumbi wa Songea Club,Mjini Songea
ajumbe wa kikao cha bodi ya Barabara kutoka wilaya ya Namtumbo wakifuatilia kikao hicho hivi leo.Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Halamshauri hiyo Steven Nana,Mkurugenzi wa Halmashauri Mohamed Maje(katikati) na Mbunge wa Namtumbo Vitta Kawawa.

Wananchi wa mkoa wa Ruvuma wametakiwa kulinda na kutunza barabara zote za mijini na vijini kwa kutong’oa au kuiba alama ,kutoharibu makaravati au vyuma ili kuzifanya barabara zidumu .

Rai hiyo imetolewa leo mjini Songea na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa huo kilichofanyika katika ukumbi wa Songea Club.

Mwambungu amewasihi wananchi kutambua umuhimu wa kutunza barabara kwani zina mchango mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya Taifa

Amewakemea na kuwaonya wananchi wenye mazoea ya kuharibu Miundombinu ya barabara kwa kutupa taka kwenye mitaro ya maji na hivyo kusababisha barabara hizo kuwa dampo la kutupia takataka badala ya kupitisha maji

“Ni muhimu kwa wananchi wetu wote kuelewa na kuchukua hatua za kutunza Miundombinu ya barabara ili ziendelee kusaidia shughuli za kiuchumi.Tuwakamate wanaong’oa au kuiba alama za barabarani,kuiba na kung’oa vyuma na makaravati ili wakipatikana wafikishwe kwenye vyombo vya Sheria” alisisitiza Mkuu wa Mkoa

Kuhusu wakandarasi wanaojenga barabara kwa viwango hafifu Mwambungu amesema serikali haitosita hata kidogo kumfukuza au kumsimamisha makandarasi yeyote katika mkoa wa Ruvuma ambaye anadhani barabara hizi ni kichwa cha mwendawazimu ambacho mlevi hujifunzia kunyoa.

Mwambungu ameaagiza wahandisi wa halmashauri za wilaya na Manispaa kutekeleza wajibu wao kwa makini na watumie utaalam wao kuifanya Miundombinu ya barabara kuwa na ubora unaostahili.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amewafahamisha wajumbe kuwa mkoa umepiga hatua kubwa ya mafaniko katika sekta ya barabara kwani jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 245 zimepandishwa hadhi kuwa za mkoa kutoka halmashauri

Amezitaja barabara hizo kuwa ni Mlilayoyo-Hanga (Km 15.1) Mtonyi- Naikesi (Km49) zote hizi zipo wilaya ya Namtumbo,zingine ni barabara ya Unyoni-Tingi-Mkenda (Km 110.7) iliyopo katika wilaya za Nyasa na Mbinga.

Barabara nyingine iliyopandishwa hadhi kuwa ya mkoa ni ile ya Mindu-Ngapa (Km 40) iliyopo wilaya ya Tunduru.

Kwa kupandishwa hadhi barabara hizi amesema zitaufanya mkoa wa Ruvuma wenye Halmashauri tano kuwa na mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 3,550.01 kutoka kilometa 3,765.01 za awali.

Kuhusu barabara za mkoa zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) zimeongezeka kutoka kilometa 1,961.74 hadi kufikia kilometa 2,176.74 za awali.
……………………………………………………………………………………………….
Na Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top