Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Balozi seif Idd awaeleza wafanyabiashara nchini umuhimu wa bima katika kuendesha biashara zao.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Waziri Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakifika eneo la Darajani katika maduka yaliyoungua moto kuwafariji wafanyabiashara waliopatwa na ajali hiyo.
Mkuu wa Makontena yaliyoungua moto Darajani Bw. Suleiman Masoud (katikati) akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif usumbufu wanaoupata kutokana na ufinyu wa maeneo ya kufanyia baiashara zao. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Bidhaa zilizoungua moto katika Duka la Bw. Abdulla Hemed Khamis liliopo Darajani Mjini Zanzibar pembezoni mwa eneo la maduka linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi Afisi Kuu Kisiwandui.
Balozi Seif akiangalia bidhaa katika maduka ya jirani na yale yaliyoungua moto ambapo wamiliki wake wamelazimika kuondoa bidhaa zao wakati wa maafa hayo ya mato.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa Wafanyabiashara Nchini kuzingatia suala la Bima katika kuendesha Biashara zao ili kujijengea umakini wakati wanapopatwa na majanga.
Ametoa sisitizo hilo mara baada ya kukagua maduka mawili yaliyoungua moto kutokana na hitilafu ya umeme pembezoni mwa eneo la maduka linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Balozi Seif amesema wafanyabiasha wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na biashara zao wakati wanapopatwa na majanga mbali mbali na kushindwa kurejesha mtaji huo kutokana na kukosa Bima.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema faraja kubwa hupatikana kwa washirika wa Bima na hii faida yake huonekana pale muhusika anapokumbwa na majanga ndani ya harakati zake za kibiashara.
Balozi Seif amewapa pole wafanyabiashara hao na kuwataka kuendelea kuwa na subra wakati huu mgumu wanaoendelea kukabiliana nao kuyokana na ajali hiyo ya moto.
Mapema Mmoja wa Wafanyabiashara walioathirika na ajali hiyo Bw. Abdulla Hemed Khamis alimueleza Balozi Seif kwamba chanzo cha moto huo kinatokana na hitilafu ya umeme iliyosababishwa na wezi waliowahi kuiba baadhi ya bidhaa za chakula siku mbili zilizopita.
“ Mimi nilifika muda mfupi kwenye duka langu baada ya kupata taarifa wakati tayari nilikuwa nimeshaondoka eneo hilo, lakini nakishukuru kikosi cha Zima moto na Uokozi Zanzibar kilichosaidia kuuzima moto huo katika kipindi kifupi sana”. Alieleza Bwana Hemd.
Bw. Hemed amesema eneo lao la biashara limekuwa likikumbwa na wizi wa mara kwa mara unaopelekea kuwavunja moyo katika harakati zao za kujitafutia riziki kupitia sekta hiyo ya biashara.
Hata hivyo Mfanyabiashara huyo wa biashara ya vyakula mchanganyiko Bw. Abdulla Hemed Khamis alishindwa kukisia hasara halisi iliyompata kutokana na moto huo.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Makontena hayo Bw. Suleiman Masuod aliiomba Serikali kushajiisha Wawekezaji kufikiria kujenga majengo makubwa ya Biashara (Shooping Mole) kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa ngazi ya kati.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top