- Kuongeza idadi ya wakaguzi wa shule
- Yapiga Marufuku Walimu Kutumia Wanafunzi Kusahihisha Madaftari ya Wanafunzi Wenzao
Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imesema itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya
kuimarisha ukgauzi wa shule ili kuhakikisha ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo
ya wanafunzi na ufundishaji shuleni.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Marystella
Wassena katika mahojiano na kituo cha Redio Uhuru cha jijini Dar es
salaam.
Wassena amesema chini ya
utaratibu na mfumo wa sasa kila shule inatakiwa kukaguliwa mara moja kila mwaka
hatua ambayo imekuwa ikitekelezwa na wakaguzi wa elimu wa kanda na wa wilaya
katika kuhakikisha maendeleo ya mwanafunzi. Hata hivyo bado kuna changamoto
katika kuzifikia shule zote.
Mkurugenzi huyo amesema
katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Wizara inakusudia kutumia
mbinu na mikakati mbalimbali ili kuongeza kiwango cha ukaguzi shuleni ikiwemo
kuongeza idadi ya wakaguzi.
“Kila shule inapaswa
kukaguliwa mara moja kwa mwaka na tumekuwa tukifanya hivyo ingawa tumeona kwamba
kuna haja ya kuongeza kiwango cha ukaguzi na kwa sasa kuna mipango inafanyika
ili kuwezesha jambo hili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.”Alisema
Wassena.
Amesema zipo nchi ambazo
shule zinakaguliwa zaidi ya mara moja kwa mwaka. Alitolea mfano wa nchi ya Korea
ya Kusini ambapo shule zinakaguliwa mara moja kila muhula, mfumo ambao amesema
unaweza pia kutekelezwa Tanzania.
Ametaja baadhi ya juhudi
ambazo Serikali inazifanya kwa hivi sasa ni kuimarisha ukaguzi wa shule kwa
kushirikiana na UNICEF kutoa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule
ili washiriki kikamilifu kukagua shule zao ikiwa ni pamoja na ufundishaji na
kuona kuwa mazingira ya shule zao yanafaa katika kutoa Elimu
bora.
“Waratibu Elimu Kata na
Wakuu wa Shule watasaidia sana iwapo kila mmoja wao atakuwa na ujuzi wa kukagua
shule zao na kufahamu namna bora ya kuondoa mapungufu yanayojitokeza kwa kuwa
wao wapo karibu zaidi na shule hizo,” alisema.
Wassena ameeleza zaidi
kuwa kumekuwa na juhudi nyingi za kuboresha ufundishaji shuleni, juhudi ambazo
zimekuwepo hata kabla ya matokeo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012 amabazo ana
imani kuwa
zitatoa
Post a Comment