Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana kulia akizungumza na Mohamed Seif Khatib
katikati na Mjumbe wa Katibu wa NEC Idara ya Oganizesheni na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Morogoro INNOCENT KALOGERIS mara baada ya kuwasili Wilayani Gairo wakitokea
Wilayani Kilosa ambako kabla ya kuondoka kulifanyika mkutano wa hadhara katika
uwanja wa Kilosa Town mjini Kilosa pia ilifanyika mikutano ya ndani ambapo
Katibu Mkuu aliongea na viongozi wa mashina, Madiwani wenyeviti, wajumbe na
waasisi wa chama hicho ikiwani pamoja na kufungua mashina katika kuimarisha
chama na kukagua baadhi ya shughuli za maendeleo, kushoto ni Nape Nnauye Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi
Kikundi cha ngoma za asili ya
kabila la Wapogolo kikicheza ngoma hiyo kabla ya kufanyika kwa mkutano wa
hadhara katika uwanja wa Kilosa Town na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali
pamoja na wafuasi wa chama hicho
Kwaya ya CCM Kilosa ikiimba
katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kilosa Town leo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi chama cha Mapinduzi
akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Kilosa Town uliofanyika
mjini Kilosa leo
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia wananchi
waliojitokeza katika mkutano huo uliofanyika mjini Kilosa leo.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha
Mapinduzi Wilayani Kilosa wakimsikiliza Ndugu Abdurahman Kinana wakati
alipokutana nao leo katika mkutano wa ndani mjini Kilosa
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na viongozi wa
CCM Wilaya ya Kilosa katika mkutano wa ndani.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi chama cha Mapinduzi
akizungumza na mmoja wa watoto waliohudhuria katika uzinduzi wa shina mjini
Kilosa
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi chama cha Mapinduzi akiwa
amekaa na akina mama kwenye mkeka huku akisaini kitabu cha wageni wakati wa
uzinduzi wa mashina mjini Kilosa.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akipandisha bendera mara
baada ya kuzindua tawi la CCM Kibaoni wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani
Kilosa leo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Datomax
Selanyika Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi wakati alipokuwa akimuelezea faida za
kuhifadhi Mbuga za wanyama na kutunza mazingira ya mbuga hizo, Datomax pia
amezungumzia mpango wa kuihamisha barabara ya lami itokayo Dar es salaam kwenda
Tunduma ambayo imekatisha katika mbuga hiyo na faida za
kuihamisha 

Post a Comment