Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar naKatibu Mkuu wa
chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa
Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya
mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa
chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa
Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya
mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa
chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akisikiza utenzi kwa
makini,kulia ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud Hamad na kushoto
Mwenyekiti wa Wilaya ya Kaskazini (A). huko Mkwajuni Kaskazini A
Unguja.
Wanachama wa CUF wakisikiliza kwa makini Maalim Seif
Sharif Hamadi hayupo pichani alipokuwa akiwahutubi katika mkutano wa hazara
uliofanyika katika viwanja vya mpira Mkwajuni.
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na
katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar
ni nchi ya biashara hivyo inataka kujitegemea iweze kupunguza ushuru ili
wananchi wapate kununua bidhaa kwa bei nafuu.
Kauli hiyo ameitoa huko katika viwanja vya Skuli
ya Mkwajuni Wilaya ya kaskazini “A” wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa
Mkoa huo.
Amesema iwapo Zanzibar itapata mamlaka yake
kamili itaweza kuwa na bandari huru, ushuru na bei za bidha
vitapungua.
“Zanzibar ni nchi ya biashara tunataka tuwe na
bandari huru ili tupate kuweka kodi ndogo na ushuru ukipungua bei za bidhaa
zitapungua”alieleza Maalim.
Aidha
amesema kuwa wananchi wanataka kuwepo kwa bandari na kupungua ushuru ili wapate
kuweka bei wanazotaka wenyewe na sio kuamuliwa na mtu
mwengine.
Akizungumzia Muungano Maalim Seif amesema
wazanzibari waliowengi wanataka serikali ya mkataba iwe na mamlaka kamili na
isiingiliwe katika maamuzi yake.
“Haya ni matakwa ya wananchi wenyewe na sio matakwa ya CUF hili ni la
wazanzibar wenyewe” alieleza Katibu huyo.
“Zanzibar
ni nchi matakwa ya wazanzibari yaheshimiwe yasiingiliwe na wengine kwani mamlaka
na madaraka hayo ndiyo yanayoweza kuyatatua matatizo ya wazanzibar” alifafanua
Maalim Seif.
Hata hivyo
Katibu huyo ameitaka Tume ya kukusanya maoni ya Katiba kuhakikisha kwamba
wajumbe waliochaguliwa kuwakilisha kutoa maoni katika Katiba hiyo wamechaguliwa
kihalali na sio kupandikizwa.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR.
Post a Comment