Wanafunzi
wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar zikiwemo Makongo, Airwing,
Mtakuja Beach na Chang'ombe wakiwa Safarini Kulekea katika ziara ya
kutembelea Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yapo kwenye
orodha ya urithi wa Dunia katika safari ya iliyoandaliwa na Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) wakati wa kumbukumbu ya Biashara ya
Utumwa na kuwaenzi waliopoteza maisha katika biashara hiyo iliyokuwa
imeshamiri katika maeneo hayo.
Biashara
hiyo ya Watumwa ilifanyika kwa miaka 400 na kuhusisha zaidi ya Waafrika
milioni 15 na watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa waathirika wa
ukatili wa Utumwa na kuendelea kuteseka na madhara yaa biashara ya
Utumwa.
Kiongozi wa msafara huo Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (wa tatu kushoto)
njiani kuelekea Kilwa Kisiwani.
Afisa
Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa ziara kwa wanafunzi baada ya
kufika katika bandari ya Kilwa kabla ya kuelekea Kilwa Kisiwani kwa
ziara ya mafunzo ya kumbukumbu za biashara ya Utumwa.
Ambapo
alisema lengo la ziara hiyo ni kutaka Wanafunzi kujifunza madhara ya
biashara ya Utumwa jinsi ilivyofanyika na madhara yake na ili waweze
kusaidia katika jitihada za kuitokomeza biashara hiyo ambayo mpaka sasa
bado inaendelea kufanyika kimya kimya katika maeneo mbalimbali nchini na
kuwataka kuzijua haki zao za kibinadamu na kutogeuzwa bidhaa za kuuzwa
kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa udanganyifu wa kupelekwa kufanya
kazi nchini za kigeni.
Mwl. Mwasi wa shule ya Sekondari Chang'ombe (mwenye nyekundu) akiwa ndani ya boti na wanafunzi kuelekea Kilwa Kisiwani.
Wanafunzi wakiwasili Kilwa Kisiwani.
Picha
juu na chini' Tour Giude' Dullah akitoa malekezo ya ramani ya sehemu
watakazotembelea wanafunzi hao ili kupata ufajamu wa jinsi Historia ya
eneo hilo ilivyokuwa hadi kufikia biashara ya Utumwa na majengo
yaliyokuwa yakitumika Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wanafunzi
wakichukua maelezo muhimu kutoka kwa Mtaalamu wa masuala ya Historia ya
Asali ya Kilwa Kiswani na Songo Mnara wakiwa kwenye makaburi
waliyozikwa viongozi waliotawala eneo la Kilwa Kisiwani.
'Tour
Giude' Dullah akiendelea kutoa ufafanuzi wa maeneo mbalimbali
yaliyotumika enzi za biashara ya Utumwa ikiwemo Misikiti, Gereza na
Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan ambaye alikuwa mtawala wa eneo hilo.
Wanafunzi wakielekea kwenye Gereza maarufu lililokuwa likitumiwa na kufunga watumwa.
Muonekano wa Gereza hilo kwa Nje Lango Kuu la kuingia.
Mhifadhi
Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said (mwenye shati la
zambarau) akionyesha Kisima kilichokuwa kikitumiwa na wafungwa ndani ya
Gereza hilo.
Wanafunzi wakiangalia Kisima kimoja wapo ndani Msikiti wakati huo.
Mmoja
ya wananfunzi wa shule hizo walioitembelea maeneo hayo ya kumbukumbu
akishangaa Mzinga uliodumu mpaka leo toka Karne ya 9 baada ya kuzaliwa
Kristo.
Mafunzo yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi hao.
Moja ya Majengo ya Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan aliyeoa wanawake 77 enzi za utawala wake.
Mhifadhi
Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said katika picha ya
kumbukumbu na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na Phillip Musiba
pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam katika
siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya Utumwa.
Wanafunzi
wakisindikizwa na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (mwenye kitenge)
kupanda boti kurudi Bandarini baada ya kuhitimisha ziara yao Kilwa
Kiswani.
Afisa
Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na mfanyakazi mwenzake Phillip
Musiba, walimu waliojumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilwa
katika ziara hiyo katika picha ya pamoja.Picha na Mo Blog.
Post a Comment