Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimkaribisha
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika
(African Union Advisory Board on Corruption-AUABC), Prof. Adolphe Lawson mara
baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mpango wa kuanzishwa
kwa Makao Makuu ya AUABC Mkoani Arusha, Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika
Wizarani tarehe 19 Aprili, 2013.
Prof. Lawson akimweleza jambo Balozi Kasyanju
wakati wa mazungumzo yao.
Prof. Lawson (kushoto) akiendelea na mazungumzo
na Balozi Kasyanju huku Bw. Benedict Msuya (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika
Kitengo cha Sheria akinukuu mazungumzo hayo.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa


Post a Comment