Viwango vipya vya nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani zimeanza kutumika jana, huku wananchi wakizipinga wakidai zinawaumiza zaidi kiuchumi.
Wakati baadhi wakilalamikia kupanda kwa nauli za dalala
katika maeneo yao, baadhi ya wafanyakazi wa mabasi yaendayo mikoani wameendelea
kutoza nauli ya zamani.
Zoezi la kupandisha nauli nchini lililoanza jana
limewagawanya wamiliki wa magari na kufanya baadhi ya safari za mikoani
kupandisha nauli, huku nyingine zikiendelea kuwa kama zamani wakati nauli za
daladala Dar es salaam zikipanda kama ilivyoagizwa.
Hatua hiyo ya kupandisha nauli ilizua tafrani baina ya
makondakta na abiria waliokuwa wakisafiri katika safari mbalimbali ndani ya
jiji, hususan wale waliokuwa hawajui kuwa jana ndiyo siku ambapo nauli
zilitakiwa kupanda.
Mwananchi liliweka kambi katika Kituo Kikuu cha Mabasi
yaendeyo mikoani cha Ubungo tangu saa 12 asubuhi na kushuhudia baadhi ya abiria
wa safari za Arusha na Kilimanjaro wakibishia kiwango cha juu cha nauli
kilichopanda, hali iliyowafanya baadhi ya abiria kutishia kususia
safari.
Hata hivyo, walilazimika kulipia kiwango hicho cha
ziada kutokana na umuhimu wa safari zao japo kwa majibizano na mawakala wa
kukatisha tiketi waliopo kituoni hapo.
Kwa mujibu wa Ofisa wa Chama cha Kutetea Abiria
Tanzania (Chakua), Gervas Rutaguzinda safari za mikoani ambazo zilipandisha bei
ya nauli ni Arusha, Moshi, Mwanza, Bukoba, Musoma na Kigoma huku nyingine
zikiendelea kama zamani.
Alisema awali nauli ya kutoka Dar es Salaam kwenda
Arusha kwa basi la kawaida ilikuwa Sh18,900 lakini jana tiketi zilikuwa zikiuzwa
kwa Sh22,700 ambapo kutokana na ugumu wa kupatikana chenji abiria walitakiwa
kulipa Sh23000.
“Nimewapokea watu watano wa kwenda Mwanza na wawili wa
safari ya Kigoma ambao walileta malalamiko kuwa walishindwa kusafiri kutokana na
kukosa ongezeko la nauli walilokutana nalo” alisema
Rutaguzinda.
Alisema baadhi ya wamiliki wa basi walibainisha kuwa
watapandisha nauli ifikapo mwezi wa sita, lakini kwa sasa wataendelea na nauli
zao za kawaida.
Naye wakala wa kukatisha tiketi kwa safari za Arusha na
Moshi aliyejitambulisha kwa jina moja la Ipiana alisema ongezeko hilo limeathiri
pato lao kwa kuwa katika nauli ya awali alikuwa akipata Sh2,000 kama kamisheni
kwa kila tiketi, lakini kwa jana fedha zote zlitakiwa kupelekwa kwa mmliki wa
basi.
Mwananchi
Mwananchi
Post a Comment