Loading...
ZITTO KABWE ALIVYOLIPANIA BUNGE LA SASA
#RBT biashara ya kuuza kazi za sanaa mfano nyimbo kama miito ya simu ie #Ringtones imeshamiri sana nchini. Unataka kujua biashara hii inaingizia mapato kiasi gani kampuni za simu (Network Providers), wachuuzi ama content providers/content aggregators na wasanii (content creators)? Unataka kujua Ni namna gani biashara hii ingeweza kuwa mkombozi wa wasanii wetu Kwa kuwaongezea kipato na hivyo kuongeza ajira nchini lakini imekuwa mnyonyaji mkubwa wa jasho la wasanii kwa kuwagawia mapato kiduchu? Unataka kujua hatua tunazopendekeza ili kuhakikisha kuna #Uwazi katika biashara hii na mgawo wa mapato unakuwa wa haki Kwa wadau wote yaani wasanii na kampuni za simu? Basi fuatilia kikao cha #Bunge cha kesho tarehe 9 Aprili 2013 kuanzia saa Tatu kamili asubuhi ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia itajibu swali la msingi na maswali ya nyongeza kuhusu biashara ya #RBT . Pia utajua kuhusu wimbo 1 tu wa #Kesho ulinunuliwa na watu wangapi katika mwezi mmoja tu wa January 2013 na mtunzi wa wimbo huo alipata mapato kiasi gani dhidi ya mapato waliopata makampuni ya simu na content providers wenye mkataba na msanii huyo. Wajibu wa kulinda wanyonge dhidi ya wenye Nguvu Ni wajibu wa Dola. Sasa Ni mwendo wa #Uwazi na #MapatoYaHaki katika kazi za Sanaa nchini kwetu.
Post a Comment