Afisa uhusiano wa CSSC Bi. Rachel
Mkundai akikabidhiwa Tuzo kutoka kwa waandaji “Gender Links”
--
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) imeshinda
Tuzo ya kutambua mchango wa mashirika ya dini katika kuwawezesha wanawake
kutambua haki ya afya ya uzazi. Tuzo hiyo imetolewa na Shirika linalotetea
masuala ya jinsia (Gender links) ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.
CSSC ilitangazwa mshindi na kukabidhiwa Tuzo hiyo
wakati wa kilele cha mkutano mkuu wa masula ya jinsia ya ukanda huo uliofanyika
nchini Afrika ya Kusini.
Mashindano hayo yalihusisha washiriki 213 kutoka nchi
13 ambazo ni wanachama wa SADC, na CSSC iliibuka mshindi katika kupengele cha
mashirika ya dini na kuwashinda wengine 13 katika kipengele hicho.
Ushindi wa CSSC umepatikana baada ya kuwasilisha makala
ya filamu (Documentary) kuhusu namna ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa kabla ya
miezi tisa (Pre-mature) kukua na kuongezeka uzito unaostahili kwa kutumia njia
ya asili maarufu kama “Kangaroo method” Njia hii inatumika katika hospitali ya
wilaya ya Sengerema inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la
Geita.
Na
Renatus
Sona
Afisa Habari
-CSSC


Post a Comment