Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma.
Picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi hao.(Picha na Juma Nyumayo)
---------------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea
SIKU moja baada ya
Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet kutangaza kustaafu nafasi
hiyo kauli ambayo ilizua maswali na mijadala mingi miongoni mwa waumini wa
kanisaa katoliki nchini na wananchi kwa ujumla ameamua kuzungumza na waandishi
wa habari mjini Songea kufafanua zaidi kuhusiana na uamuzi wake huo.
Alisema kuwa ni wazi kuwa uamuzi huo aliouchukua umewashitua
wengi lakini amelazimika kufikia uamuzi huo kufuatia kukumbwa na matatizo ya
kiafya yaliyojitokeza kwake katika siku za hivi karibuni ambayo hakuwahi
kuyapata kwa miaka mingi ya maisha yake pamoja na utume.
Askofu Mtega
aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye ataendelea kuitwa Askofu mkuu mstaafu
na amepanga kuendelea kuishi ndani ya jimbo kuu la Songea na yuko tayari kueendelea kutoa ushurikiano
kwa kiongozi mwingine atakaeteuliwa kushika nafasi hiyo huku akiiasa jamii
kuishi kwa amani na utulivu na kuepuka kubaguana kwa misingi ya dini,ukabila na
itikadi za kisiasa bali waweke moyo wa uzalendo wa taifa mbele.
Alisema kuwa ameona ni vyema akakaa pembeni ili aweze kupata
muda mzuri wa kupumzika na kupata matibabu ili afya yake ikitengamaa aweze kuwa
mashauri mzuri kuliko kuendelea kunga’ang’ania mpaka afikike hatua ya kupoteza
kumbu kumbu na kuwa kikwazo na hoja ya jimbo kuzorota katika siku za mbele.
Akijibu maswali ya
baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na mambo ambayo angependa ayaone
yakifanyika alisema kuwa suala la elimu nchini siyo la kulipuuza na linapaswa
kuwekewa misingi mizuri na imara kuanzia ngazi ya elimu ya msingi kwa sababu
utaratibu uliopo wa kufanyia marekebisho alama za wahitimu waliofeli katika
mitihani haulisaidii taifa kielimu pamoja na uhifadhi wa mazingira ambayo
yanaendelea kuharibiwa kwa kasi kubwa na jukumu la kuvinusuru hivyo vyote ni la
kila mmoja kwa maslahi ya taifa.
Aidha aliwataka
viongozi wa kanisa katoliki jimboni humo kujikita zaidi katika kuimarisha imani
kwa waumini katika kanisa hilo ambalo yeye amelitumikia kwa kipindi cha miaka
22 na Jimbo la Iringa ambalo alilitumikia kwa kipindi cha miaka sita ambalo kwa
sasa linaongozwa na Askofu Tarciusi Ngalalemkutwa ambaye sasa ataliongoza pia
jimbo kuu hilo la Songea linaloachwa na Askofu Mtega.
Mwisho.
Post a Comment