Na Brandy Nelson, Mwananchi
Wanafunzi 15, wa Shule
ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe mkoani Mbeya
, wanashikiliwa polisi kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la wanafunzi wa
kiume na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.
Aizungumzia tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku
shuleni hapo na kwamba wanafunzi hao walifikia hatua hiyo ya kuchoma
moto bweni hilo, wakipinga kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wenzao
watatu kwa utovu wa nidhamu.
Aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa
utovu wa nidhamu kuwa ni Joseph Robert (18), anayesoma kidato cha nne na
Mwita Chacha (17) na anayesoma kidato cha tatu, wote wakazi wa Kitunda
jijini Dar es Salaam na Mwingine ni Daniel David (18), anayesoma kidato
cha tatu ambaye ni mkazi wa Ipinda wilayani Kyela.
Alisema kuwa wanafunzi hao watatu waliwahamasisha
wenzao kuwaunga mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kwamba
bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi 50, ambao hawakuwa
tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Post a Comment