Zawadi Msalla-MAELEZO DODOMA
Serikali
imeuagiza mfuko wa Bima ya Afya kubadilisha mfumo wa vitambulisho vya
Bima ya Afya ili kuongeza uthibiti wa udanganyifu unaofanyika ndani ya
mfumo uliopo.
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Seif
Seleman Rashidi alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Mariam
Kisangi (CCM Viti Maalumu) na kuongeza kuwa Wizara inafahamu udanganyifu
unaofanyika hivyo inashirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya ili
kuhakikisha udanganyifu huo una dhibitiwa.
Ubadilishaji
wa mfumo huo pia umelenga katika kubadilisha vitambulisho vya sasa ili
kuwa na aina bora zaidi inayotumia teknolojia mpya ya utambuzi na
kuimarisha usimamizi wa huduma katika vituo vilivyosajiliwa na Mfuko
hasa vituo vikubwa vilivyopo Dar es Salaam.
Alisema
baadhi ya wanachama wamekuwa sio waaminifu kwa kuuza nafasi zao au
kuingiza majirani badala ya kujaza wategemezi wanaostahili kisheria
.Aidha alisema wapo wanaoshirikiana na watoa huduma wasio waaminifu na
kuingiza watu wenye magonjwa sugu na yenye gharama kubwa na kutolea
mfano wa magonjwa ya saratani.
Naibu
Waziri alisema kwa mfumo wa sasa eneo la wategemezi linalenga
wategemezi halisi wa wanachama kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa
Umma.
Hata
hivyo alisema Mfuko huo uko makini katika kuhakikisha unatoa huduma
stahili kwa wateja wake na kwa wale walioandikishwa kama wategemezi hadi
pale utaratibu mpya utakapopitishwa rasmi .
Akieleza
manufaa ya mfuko huo alisema msingi mkubwa wa Bima ya Afya za Jamii ni
kuwezesha mwanachama kutibiwa kulingana na tatizo au ugonjwa unaomsumbua
bila kujali michango yake.
Alisema
dhana ya bima ya afya imejengeka katika misingi ya kuchangiana ,ambapo
mwenye familia ndogo bila wategemezi anawasaidia wenye familia kubwa .
Mwenye mshahara mkubwa husaidia wenye mishahara midogo na vijana
wanawasaidia wazee.
Aidha
Dkt.Seif alisema Wizara inasubiri ushauri kutoka ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutoa elimu kwa
wananchi juu ya umuhimu wa Bima ya Afya na utendaji kazi wa vitambulisho
hivyo.
Post a Comment