KAMANDA
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi
wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake kuhusiana na tukio la moto.
*********
Na Nathaniel Limu.
Vibanda
vinne vya biashara vinavyozunguka soko kuu la Manyoni mjini mkoa wa
Singida, vimeteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mamalishe
kusahau kuzima moto wakati akifunga biashara yake.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela amesema mtu wa kwanza
kuuona moto huo ulioanzia kwenye kibanda cha mama lishe, ni mlinzi wa
soko hilo aliyejulikana kwa jina la Jotamu Daud.
Kamanda
huyo amesema moto huo baada ya kupamba zaidi, ulihamia kwenye vibanda
vingine vya maduka ya nguo na kuteketeza vibanda hivyo na mali yote
iliyokuwa ndani.
Kamanda
Kamwele ametoa wito kwa mamalishe na babalishe kuhakikisha wanazima
majiko yao ya moto mara tu wanapomaliza kufanya biashara zao ili
kuzuia uwezekano wa kuwaka wakati wao hawapo.
Post a Comment