Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waumini wengi wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea washitushwa na kujiuzulu kwa Askofu Mtega



 Waumini wa kiwa njia panda wakingoja kauli ya Uhakika kuhusu Mhashamu Norbet Mtega ni kweli Amestahafu ? 
 Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.
.....................................................
Na Nathan Mtega,Songea.

BAADHI ya waumini wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea  waishio katika  maeneo mbali mbali  mjini Songea mkoani Ruvuma wameonesha kushitushwa na taarifa zilizo patikana za kujiuzulu kwa kiongozi  mkuu wa jimbo kuu la Songea , Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.

Taarifa za kujiuzulu kwa kiongozi huyo zilipatikana jana  majira ya saa 7 mchana ambazo zilieleza kuwa Askofu Mtega alikuwa ametembelea abasia ya wabeneditini iliyopo  Hanga wilayani Namtumbo mkoani humo .

Mhashamu Askofu Mtega alipokuwa katika abasia hiyo ya Hanga aliwatangazia waumini pamoja na watawa wa shirika la wabeneditini  kuwa kuanzia sasa yeye siyo Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea na badala yake jimbo hilo litashikiliwa na Askofu wa jimbo la Iringa Taricisius Ngalalekumtwa ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la maskofu Tanzania mpaka pale atakapopatikana kiongozi mwingine wa kushika. Wadhifa huo.

Kwa mjibu wa kiongozi mmoja wa parokia ya kanisa hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini akiongea na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu alisema kuwa ni taarifa za kweli kuwa Mhashamu Askofu Mtega ametangaza kujiuzulu wadhifa huo  na kuwa hata wao hawajui kilimkuta nini maana hata hajawahi kudokeza kuhusiana na jambo hilo.

 “Watumishi wote hatukujua kinachoendelea tumeshangazwa kuwa Askofu Mtega anatamka kwa kinywa chake kuwa yeye kuanzia sasa siyo Askofu Mkuu wa Jimbo hili la Songea jambo ambalo wote tulibaki midomo wazi na hatujui kuwa kuna nini.”alisema mtumishi huyo.

  Askofu huyo alilipokea jimbo hilo na kuliongoza baada ya aliyekuwa  Askofu wa jimbo hilo marehemu Jacobo Komba kufariki dunia .

       MWISHO.
 
Chanzo:demashownews blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top