HALMASHAURI za wilaya nchini
zimeagizwa kuunda mabaraza ya wafanyakazi ili kuweza kuyapatia ufumbuzi
malalamiko ya wafanyakazi sehemu za kazi na kuboresha utendaji wenye
kuleta tija..
Amesema baraza la majadiliano
katika sekta ya serikali za mitaa lina jukumu kubwa la kuishauri
serikali kuhusu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mamlaka za serikali
za mitaa ,ikiwemo masuala ya utumishi,.mifumo,sheria, taratibu na miundo
mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za mamlaka za serikali za mitaaa.
Waziri Ghasia,amesema
halmashauri ambazo hazijaunda mabaraza hayo kuhakikisha zinayaunda, na
yale ambayo yamemaliza muda wake wanachaguliwa wajumbe wapya na
kuhakikisha mabaraza yote yanakaa vikao ili kuweza kutatua malalamiko ya
wafanyakazi.
”Kama tunavyofahamu baraza la
majadiliano ya pamoja katika utumishi wa umma ni chombo kilichoundwa
kwa sheria ya bunge namba 19 ya 2003 ambayo ina lengo la kuimarisha
mahusiano na mawasiliano yenye tija baina ya serikali na halmashauri
ambazo hazijaunda mabaraza hayo kuhakikisha zinayaunda, nay ale ambayo
yamemaliza muda wake wanachaguliwa wajumbe wapya na kuhakikisha mabaraza
yote yanakaa vikao ili kuweza kutatua malamiko ya wafanyakazi”alisema
waziri.
Akasema kuwa baraza la
majadiliano katika sekjta ya serikali za mitaa ni chombo halali kwa
mjibu wa kifungu namba 4 (10) ( c) cha sheria iliyoanzisha baraza hilo
la majadiliano ya pamoja katika utumishi wa Umma.
Waziri,Ghasia, amesisitiza
usimamizi wa rasilimali watu katika Sekta za Umma ni suala linalotakiwa
kupewa kipaumbele kwani matumizi mazuri ya rasilimali watu ndiyo
yanayoweza kuleta matokeo mazuri katika kusimamia rasilimali nyingine
zote.
Hivyo wanalo jukumu la
msingi la kuhakikisha wanatoa ushauri kwa serikali na watumishi a sekta
hiyo ili kuongeza ufanisi wenye tija katika kuwahudumia wananchi
hivyo watumie kikao hicho kuainisha maeneo yenye changamoto zaidi kwa
watumishi ili kuondoa manung’uniko ya watumishi.
Awali mwenyekiti wa baraza
hlo jipya la kitaifa, Paulo Chikila, amesema kuwa Baraza hilo litakuwa
madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu akasisitiza kuwa mabaraza yote
lazima yafanye kazi ili kuondoa malamiko ya wafanyakazi
Post a Comment