Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama
Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo
cha watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati
alipokitembelea kituo hicho tarehe 6.6.2013. Mama Salma yupo nchini
Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku
mbili nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi. 

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na uongozi wa
kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu cha Pertapis
kilichoko nchini Singapore.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo
wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha
kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko
Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013. Kushoto kwa Mama Salma
ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu
wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis
kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013.

Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama
Sahnim Sokaimi, Mkuu wa kituo cha kurekebisha tabia za wanawake na
wasichana watukutu cha Pertapis kilichoko nchini Singapore mara baada ya
kukitembelea tarehe 6.6.2013.

Post a Comment