Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza wakati
kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss Kinondoni
2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont, jijini Dar es Salaam. Kutoka (kushoto) kwa Albert ni Katibu
Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega,
mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta, wakiwa pamoja muandaaji wa
mashindano hayo Dennis Ssebo.
Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega, akizungumza na warembo
wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 wakati Kamati hiyo,
ilipowatembelea kambini kwao. Lundenga aliwaasa washiriki hao kuongeza
bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika fainali yao.
**********************************************
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
KAMATI
ya Miss Tanzania, ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga, jana
iiliwatembelea warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013, katika kambi yao
ili kujua maendeleo ya kambi hiyo kuelekea kinyang'anyiro hicho cha
kuwania tahi la Redd's Miss Kinondoni Talent linalofanyika leo alhamisi
katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandhishi wa habari hizi, mratibu wa shindano hilo, Dennis Ssebo
alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na
kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo
ambalo litafanyika kesho Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya
Golden Tulip.
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa
wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo
mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy
Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha
WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media
Group, SufianMafoto Blog, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog,
Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com,
JestinaGeorge Blog, , Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO
Blog na Kajunason Blog.
Post a Comment