Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Leonidas Gama akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja
iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA
ikiwahusisha wakuu wa mikoa na makatibu
tawala
wa mikoa ya Manyara,Tanga,Arusha na Kilimanjaro.
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano
kanda ya kaskazini mhandisi Aneti Matindi akiteta jambo na injinia
wa masafa wa TCRA ,Sadath Kalolo wakati wa semina ya wakuu wa
mikoa ya kanda ya kaskazini.
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano
kanda ya kaskazini mhandisi Aneti Matindi akiwasilisha mada wakati
wa semina ya wakuu wa mikoa ya kanda ya
kaskazini.
Mkuu wa mkoa wa ManyaraEraston
Mbwilo akichangia mada katika semina hiyo
Naibu mkurugenzi wa shughuli za
Kanda wa TCRA Victor Nkya akiwasilisha
mada
katika semina hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Chiku
Gallawa pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo wakifuatilia kwa
makini mada iliyokuwa ikitolewa wakati wa semina iliyoandaliwa
na TCRA kwa wakuu hao wa mikoa ya kanda ya
ksakazini.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa
Mwilongo akichangia mada katika semina hiyo.
Meneja mawasiliano wa mamlaka ya
mawasiliano TCRA wa kanda ya kaskazini Innocent Mungi akitoa
mada katika semina hiyo.
Washiriki
katika picha ya pamoja.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
SERIKALI imetoa wito kwa mamlaka ya mawasliano Tanzania TCRA kuangalia namna ya kupata mbinu mpya za kisasa katika kudhibiti wale wachache wanaojaribu kutumia teknolojia hiyo kuvunja umoja ,amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha wakuu wa mikoa fanyika katika hotel ya Sarsalenero iliyopo mjini Moshi na kuwashirikisha wakuu wa mikoa pamoja na makatibu tawala wa mikoa ya Arusha,Tanga,Manyara na Kilimanjaro.
Gama alisema matummizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano sanjari na uwepo wa tovuti na Wavuti zinazo kiuka kuharibu mila,destuli na maadili ya mtanzania ni miongoni mwa changamoto zinazo ikabili sekta hiyo kwa sasa .
Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na simu za mkononi katika kueneza fitna,chuki,matusi na uhasama miongoni mwa jamii ya watanzania jambo ambalo alisema TCRA inapaswa kuengalia eneo hilo kwa makini zaidi ili mitandao hiyo isije ikatumika katika kuwagawa watanzania.
Alisema ukuaji wa shughuli za kiuchumi zinazohusiana teknolojia ya mawasiliano ya habari zinaongezeka kwa kasi kubwa kanda ya kasikazini na kuwa kichocheo kikubwa katika sekta za Kilimo ,utalii na biashara katika mikoa ya kanda ya kaskazini sambamba na kupatikana kwa fursa mpya za ajira.
Awali akieleza malengo ya semina hiyo naibu mkurugenzi wa shughuli za kanda wa TCRA, Victor Nkya alisema mamlaka ya mawasiliano imelenga kujitangaza na kuwaelimisha wakuu wa mikoa juu ya shughuli za mamlaka hiyo ili kutambua haki na wajibu kama watumiaji wa mawasiliano.


Post a Comment