Flaviana Matata akiwa katika pozi
.Ashika nafasi ya juu Afrika na Kimataifa kwa kipato
Na Mwandishi Wetu
NYOTA
ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi
kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa
upande kipato.
Kwa
mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika
(Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee
aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na
kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika
orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba
moja na wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa
kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali
ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni
Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak
Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.
Flaviana
Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania
mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza
muda wake aliendelea na fani ya uanamitindo Afrika kusini na baadaye
alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni
makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko
Wilhelmina Models.
Akizungumza
kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo
ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha
kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na
nchi yangu”.
Post a Comment