Makao
Makuu ya kituo cha habari na mawasiliano cha Redio ya jamii Sengerema
Fm mkoani Mwanza kunakofanyika warsha ya wiki moja kwa redio za jamii
nchini kwa ajili ya kuziandaa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Meneja
wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Radio Sengerema mkoani Mwanza
Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa
Wakurugenzi na Mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya
wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO kupitia mradi wa DEP kwa ajili ya
kuwaanda kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea
uchaguzi wa mwaka 2015.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumza na mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania nchini katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya mradi wa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Mshauri
wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo
kwa washiriki wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani
Sengerema mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mradi wa DEP
kutoka UNESCO Courtney Ivins, Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al
Amin na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti
kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy.
Meneja
wa Redio Sibuka Fm Maswa Bi. Bhoke Okachu akiwasilisha maoni wakati wa
kujadili mradi wa DEP kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
Picha
juu na chini ni Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa
redio za jamii 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaohudhuria warsha
hiyo.
Meneja wa Kyela Fm Lucas Kulwa akichangia maoni yake wakati wa warsha hiyo.
Na. Mwandishi wetu
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limesema
kwamba linakusudia kuvijengea uwezo vyombo vya habari vya jamii ili
kuviwezesha vyombo hivyo kuandaa vipindi vya elimu kuhubiri mijadala ya
Amani na Demokrasia (DEP) kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin
amesema UNESCO, UNDP, UN WOMEN, wamekusudia kufanya hivyo kwa dhamira
ya kuvitayarisha vyombo hivyo mapema baada yakuona changamoto nyingi
zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo elimu ya kutosha
haikuwafikia wananchi waliowengi.
Yusuph
ameyasema hayo katika kituo cha habari na mawasiliano cha Redio
Sengerema mkoani Mwanza, wakati akiwasilisha mada ya amani na demokrasia
kwa mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania, wasimamizi wa
redio za halmashauri na mazingira Tanzania bara katika warsha ya wiki
moja juu ya matayarisho ya redio hizo katika uchaguzi ujao.
Uhamasishaji
wa elimu ya wapiga kura, usawa wa kijinsia katika kuhamasisha kinamama
kushiriki katika uchaguzi kwenye kujiandikisha, kupiga kura nakujitokeza
kugombania nafasi mbalimbali za uongozi na kutoyafikia makundi maalum
ipasavyo licha ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa ukilinganisha na muda
mchache wa elimu uliotumioka kabla ya uchaguzi ni mambo muhimu
yaliyohamasisha elimu hio kutolewa mapema Yusuph alisema.
Amebainisha
kuwa katika kuhakikisha ufanisi mkubwa unafikiwa katika uchaguzi ujao,
wameongeza redio shiriki kutoka 12 hadi 25, huku manufaa zaidi
yakielekea visiwani ambapo redio ya jamii Tumbatu na redio jamii kusini
Pemba, zitaanzishwa na redio Uvinza mkoani Kigoma ambazo kwa pamoja
zitapewa mafunzo yakutosha ikiwa ni pamoja na viongozi wa bodi, watu
mashuhuri, viongozi wa halmashauri na viongozi wa dini.
Al
Amin amesema kutokana na uzoefu, chaguzi zilizopita katika nchi jirani
na matokeo yake, uchaguzi ujao huenda kukawa na changamoto nyingi, hivyo
ni vyema kuhamasisha majadiliano ya amani yatiliwe mkazo na kuboresha
mawasiliano na taasisi husika ambapo watendaji 250 wa habari watapewa
mafunzo na watanzania milioni nane watafikiwa kupata taarifa kupitia
redio za jamii.
Amesisitiza
kuwa kazi ya kuhubiri amani na demokrasia inahitaji kuvumiliana
kutokana na changamoto zilizopo na kuwa vyombo vya habari, ni vyema
kujua miiko na usawa katika utendaji hasa katika kuandika na kutangaza
taarifa zinazohusu uchaguzi, huku akivilaumu vyombo vya habari kwa
kuhubiri uajibikaji kwa wengine, bali wao wamekuwa na mapungufu mengi na
hawanabudi kufanya marekebisho mapema.
Amesema
vyombo vya habari vya jamii, huu ni wakati muafaka wa kufanya
mabadiliko katika watendaji wake kutokana na idadi ndogo ya watangazaji
na waandishi na maripota wanawake kupungua siku hadi siku, kuboresha
vipindi na kufahamu kuwa utamaduni wa watanzania ni amani na vyema
kudumisha utamaduni huo kuanzia vyombo vya habari vya jamii.
Post a Comment