TAMASHA
la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika
Septemba 8 katika viwanja vya General tyre Arusha na kushirikisha
waandishi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro na mkoa wa
Manyara.
Tamasha hili, ambalo hufanyika kila mwaka, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL).
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za
michezo mkoa wa Arusha(TASWA) Mussa Juma, alisema zaidi ya waandishi
wa habari na wadau wa habari 500 wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha
hilo.
Juma
alisema kwa upande wa michezo timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka
jijini Dar es Salaam, TASWA Arusha, Radio Sunrise, Radio 5, Radio
Triple A, Arusha One Radio na Chuo cha Uandishi wa habari Arusha ambao
ndio mabingwa watetezi.
Alisema
pia kutakuwa na timu ambazo zimealikwa ambazo ni timu ya TBL Arusha
ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, timu ya Wazee Klabu,Kitambi
Noma, Timu ya Pepsi na timu ya NSSF Arusha.
Juma
alisema katika tamasha hilo, ambalo huandaliwa na TASWA na kampuni ya Ms
Unique, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku,
mpira wa mikono na mbio za magunia.
Alisema
Septemba 7 bonanza hilo, litatanguliwa na semina ya siku moja kwa
waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na sheria za michezo,
masuala ya afya na jinsi ya kutumia michezo katika kutangaza utalii.
Hata hivyo, Juma alisema bado wadhamini wanaombwa kujitokeza kudhamini tamasha hilo.
Post a Comment