Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Wajumbe
wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia
ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa imelipongeza Jeshi la Polisi kwa
jinsi linavyotekeleza majukumu yake kwa kuwachukulia hatua wachochezi
wanaotumia mgongo wa siasa au dini hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma aliyasema hayo jana wakati wa
ziara ya kamati hiyo ilipotembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa
lengo la kujifunza na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na
uhalifu pamoja na kuboresha maisha ya askari Polisi.
Alisema,
Jeshi la Polisi linapaswa kutomuonea muhali mtu yeyote ama taasisi
itakayotumia mwamvuli wa siasa au dini kupandikiza na kueneza chuki
ndani ya jamii kitendo ambacho hupelekea uvunjifu wa amani.
Aidha,
Mwenyekiti wa kamati hiyo, alishauri kuwa viwanja vyote vinavyomilikiwa
na Jeshi la Polisi vipatiwe hati miliki ili kupunguza uvamizi katika
maeneo na viwanja vya Polisi na endapo kuna wavamizi wowote wachuliwe
hatua za haraka.
Kwa
upande wake Kamishina wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP)
Paul Chagonja alibainisha matishio yanayoikabili nchi kwa sasa ambayo
ni misimamo mikali ya kisiasa, migogoro ya wafugaji na wakulima,
biashara ya dawa za kulenya, mauaji yanayosababishwa na imani za
kishirikina na watu kuwania mali pamoja na ajali za barabarani
zinazosababisha vifo kutokana na waendesha pikipiki na kuongeza kuwa
Jeshi la Polisi limejipanga na linaendelea na mikakati mbalimbali ya
kiusalama katika kukabiliana na matishio hayo ikiwemo kupeleka askari
katika tarafa ili kuimarisha ulinzi ngazi ya tarafa hadi familia.
Aidha,
aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu
waliopo kwenye jamii kabla hawajatekeleza adhima yao ya kutenda uhalifu.
Aliongeza
kuwa hivi sasa Jeshi hilo linaendelea kutekeleza program ya maboresho
ili kuboresha vitendea kazi pamoja na maslahi ya askari ambapo kila
askari hivi sasa pamoja na mambo mengine anapata matibabu kwa kutumia
bima ya afya na zaidi ya shilingi bilioni 42 zimekopeshwa kwa askari
kupitia chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi (
Ura Saccos) kwa lengo la kuboresha maisha ya askari binafsi.
Post a Comment