Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo akitoa hotuba kwa
niaba ya mgeni rasmi baada ya ufungua rasmi Kikao cha siku mbili cha
Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu ambaye alimwakilisha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.
Elisante Ole Gabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. Suleiman Ling’ande
akitoa maneno machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa mgeni rasmi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ole
Sante Grabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
Mshauri
Mwelekezi Bw. Ernest Omalla (aliyesimama) akitoa maelezo machache kabla
kumkaribisha Mshauri Mwelekezi mwenzie Bw. Martin Cuff (kushoto) kwa
ajili ya kutoa somo kwa washiriki katika ukumbi wa TCRA leo jijini Dar
es Salaam.
Mshauri
Mwelekezi Bw. Ernest Omalla akitoa somo fupi juu ya Kikao cha siku
mbili cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu uliofunguliwa
jana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi Joyce Fissoo kwa niaba ya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Elisante Ole Grabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo (kulia) akimsomea
maelezo muhimu Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon
Mwakifwamba (kulia) mara baada ya kukamilisha kutoa hotuba fupi ya mgeni
rasmi ambaye alimwakilisha.
Baadhi
ya Washiriki waliohudhuria uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Filamu
wakifuatilia somo toka kwa wadau mbalimbali wa TAFF pamoja na Washauri
Waelekezi wakati wa uzinduzi Kikao cha siku mbiloi cha Wadau wa Filamu
kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu kilichofanyika jana katika ukumbi wa
TCRA jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Post a Comment