Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo
barua kama ishara ya Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika
tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi
hiyo, hivi karibuni nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki
Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe,
Bibi. Pili Said Kitwana.
Nguli
wa Muziki wa Dansi, Mzee Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti)
akiwa na watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
walipomtembelea nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi
karibuni. Serikali kupitia Wizara hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo
kutambua mchango wake katika tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa
kustaafu kazi hiyo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili
Said Kitwana na wa Pili Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara
Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce Hagu.
Picha zote na Concilia Niyibitanga
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
………………..
Na Concilia Niyibitanga- WHVUM
Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imempongeza Mzee
Muhidini Gurumo kwa mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki
nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo.
Akiwasilisha
barua ya Serikali ya kutambua mchango wa nguli huyo juzi nyumbani kwake
Makuburi Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi.
Lilly Beleko amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wake
katika muziki wa Dansi hapa nchini.
‘Serikali
inathamini mchango wako katika Muziki hapa nchini na itaendelea
kuzienzi kazi hizo na inakupongeza kwa kazi nzuri ulioifanya ya
kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha jamii’. Amesema Bibi. Beleko.
Naye
Rais wa Shirikisho la Muziki nchini, Bw. Addo Mwasongwe, amesema kuwa
Shirikisho linampongeza kwa kazi zake nzuri na litaendelea kumtumia
katika kazi za muziki ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri katika tasnia
hiyo.
Nguli
huyo wa muziki wa dansi nchini katika enzi zake za uimbaji ametunga
nyimbo za kuelimisha jamii kufanya kazi kwa bidii, kudumisha usawa,
amani na kuwakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto
katika maadili mema.
Mzee
Gurumo ambaye ameanza kazi ya muziki mnamo miaka ya 1960 na kustaafu
kazi hiyo mwaka huu amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kutambua kazi
yake na amefarijika kwa kukabidhiwa barua ya kumtambua na kumpongeza kwa
kustaafu kazi hiyo.
Post a Comment