THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya juzi, Jumanne,
Septemba 24, 2013, ameendesha kikao chake cha kwanza kama Mwenyekiti wa Kamati
ya Viongozi wa Nchi za Umoja wa Afrika Kuhusu Mazingira (CAHOSCO).
Rais Kikwete aliendesha
kikao hicho kwenye Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika
Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Ubalozi wa Kudumu wa AU una hadhi ya
watazamaji katika UN.
Rais Kikwete
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Nchi Wanachama wa AU
mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu Mazingira kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mheshimiwa Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia
aliyefariki na kuzikwa Septemba, mwaka jana, 2012.
Kikao hicho
kilihudhuriwa na nchi zote wanachama wa Kamati ya Mazingira ya AU ikiwa ni
pamoja na Mozambique ambayo iliwakilishwa na Mheshimiwa Rais Armando Guebuza,
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Haile Mariam Deselengy pamoja na mawaziri na
wawakilishi wa nchi za Algeria, Uganda, Senegal, Swaziland, Mauritius na
Jamhuri ya Congo.
Kikao hicho kilikuwa
kinajadili namna ya kukubaliana kuhusu msimamo wa Afrika utakaowakilishwa
katika Mkutano wa Dunia wa Mazingira wa Novemba mwaka huu nchini Poland.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Septemba, 2013
Post a Comment