. Ni Anas al-Liby alishambulia balozi za Marekani 1998
Anas
Al-Liby aliyekamatwa na wanajeshi wa Marekani mjini Tripoli kwa
kuhusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Marekani mwaka
1998 amekausha madai ya ugaidi dhidi yake.
Abu Anas al-Liby, ambaye jina lake halisi ni Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, alikanusha madai dhidi yake kupitia kwa wakili wake.
Duru
za kiusalama zinasema Anatuhumiwa kwa kuwa na uhusiano na kundi la
kigaidi la al-Qaeda na kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi
za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.
Katika mashambulizi hayo zaidi ya watu 220 walipoteza maisha yao.
Bwana Liby, mwenye umri wa miaka 49, alisemekana kuwa na kesi ya kujibu mwaka 2000.
Siku ya Jumanne Liby alionekana akiwa amefungwa pingu mkononi katika mahakama moja mjini New York.
Liby, alisikiza kwa maakini jaji akimusomea mashitaka dhidi yake .
Baadaye alikanusha madai hayo dhidi yake na jaji akaakhirisha kesi hiyo hadi Oktoba 22.
Mshukiwa aliondoshwa mahakamani baada ya jaji kusema muwa lazima aendelee kuzuiliwa kwani kuna tisho la yeye kutoroka.
Kumekuwa
na ghadhabu nchini Libya tangu makomando wa Marekani kumkamata al Liby
anayedaiwa kuwa mmoja wa viongozi wa kundi la Al Qaeda mjini Tripoli
mapema mwezi Oktoba.
Wengi walikiona kitendo hicho kama cha kutoheshimu uhuru wa Libya.
Hata
hivyo Marekani kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje John Kerry
imesema kuwa Liby alikuwa mshukiwa halali aliyepaswa kukamatwa.
Hata hivyo serikali ya Libya baada ya kukamatwa kwa Liby ilimtaka balozi wa Marekani nchini humo kueleza kwa nini ilifanya hivyo
Waziri
mkuu wa Libya Al Zeydan ambaye alitekwa nyara kwa masaa kadhaa siku
chache baada ya Al Libya kukamatwa, amesema kuwa wahalifu wenye uraia wa
Libya wanapaswa tu kushitakiwa na kuhukumiwa ndani ya nchi hiyo
Majasusi
walimuhoji Libya kwenye mali ya kijeshi kwa wiki moja kabla ya
kumpeleka mahakamani huku wanawe wakisema kuwa serikali ilihusika katika
kukamatwa kwake, madai ambayo serikali imekanusha.
Chanzo BBC



Post a Comment