
--
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi (Eng.) Bashir J. Mrindoko kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kwa
kumpandisha cheo kutoka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Mhandisi Mbogo
Paulo Futakamba, Naibu KatibuMkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwenda
Wizara ya Maji kujaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Bashir Mrindoko.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, Jumanne,
Oktoba 15, 2013, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa vile
vile Rais Kikwete amemteua Mhandisi Raphael Leyan Daluti kuwa Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuchukua nafasi ya Mhandisi Futakamba.
Kabla ya uteuzi
wake, Mhandisi Daluti alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji
na Huduma za Ufundi katika Wizara hiyo ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Balozi Sefue amesema katika taarifa yake kuwa
uteuzi na uhamisho huo umeanza Oktoba 13, mwaka huu, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Oktoba, 2013

Post a Comment