Mkuu
wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba (kushoto) akiteta jambo na mmoja
kati ya watenda kazi wa NHIF Iringa nje ya ukumbi wa RC Makambako
Utambulisho wa wageni mbali mbali waliofika katika warsha hiyo ukifanyika
Washiriki wa warsha hiyo ya mfuko wa Afya ya jamii mjini (TIKA) mjia Makambako leo
Meneja
wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Iringa Emmanuel
W. Mwikwabe akieleza faida ya TIKA mbele ya washiriki
Sekretarieti ya NHIF
Kaimu
meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Iringa
Emmanuel W. Mwikwabe (kulia ) akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya
mkuu wa mkoa wa Njombe kepten Mstaafu Asser Msangi kushoto leo nje ya
ukumbi wa RC Makambako
Mwakilishi kutoka TAMISEMI Edwin Mgendera mkurugenzi msaidizi idara ya huduma na sheria akijitambulisha rasmi
Mkuu wa mkoa wa Njombe Bw Msangi katikati akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbali mbali ya washiriki
Na FrancisGodwinBlog,Njombe
serikali
ya mkoa wa Njombe iimewataka wanasiasa katika mkoa huo
kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii
(CHF) unaowalenga wananchi wa vijijini na ule wa tiba kwa kadi (TIKA)
kwa mijini
Mkuu wa mkoa wa Njombe kepteni mstaafu Asseri Msangi alitoa ratiba hiyo mara baada ya kufungua warsha warsha ya uanzishaji wa mfuko wa afya ya jamii mijii (TIKA) katika mji wa Makambako mkoani Njombe kwenye ukumbi wa RC mjini Makambako mkoa wa Njombe leo
Alisema
kuwa serikali kjupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii
imeandaa mfumo huo wa tiba kwa jamii ili kuisaidia jamii kuweza
kupata matibabu pale inapopatwa na matatizo ya kifya na kuwa katuka
nchi zote duniani hakuna nchi hata moja ambayo inatoa bure huduma
za afya kwa wananchi wake ukiacha nchi ya Libya ambayo ilikuwa ikitoa
bure matibabu ila kwa sasa huduma hiyo katika nchi hiyo pia haipo.
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa aliwataka madiwani katika kuweka usawa
mzuri katika uchangiaji wa huduma za afya kupitia huduma hiyo
tiba kwa kadi ili kuwawezesha wananchi wengi kujiunga na mpango
huo.
Kaimu
meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Iringa
Emmanuel W. Mwikwabe akielezea juu ya makusanyo ya NHIF katika
mkoa wa Njombe alisema kuwa kwa mwaka 2012/2013 kiasi cha Tsh
milioni 428 zimekusanywa katika wilaya ya Makete ,Njombe mji na
Halmashauri ya wilaya ya Njombe pamoja na Ludewa.
Alisema
kuwa fedha hizo ni makusanyo ya mfuko wa NHIF na CHF ambapo katika
wilaya ya Makete jumla ya Tsh milioni 70.2 za NHIF zilikusanywa na
Tsh milioni 28 za CHF zilikusanywa na kufanya jumla kuu kwa wilaya
hiyo kufikia Tsh milioni 98.2.
Wakati
wilaya ya Ludewa makusanyo ya NHIF ilikuwa ni Tsh miliioni 78 na
CHF ilikuwa ni Tsh milioni 47 na kufikisha jumla ya Tsh milioni 125
na wilaya ya Njombe mji makusanyo ya CHF ilikuwa ni milioni 1 na NHIF
ilikuwa ni kiasi cha Tsh. milioni 94.8 na Halmashauri ya Njombe
fedha za CHF ni Tsh.milioni 2 na NHIF ilikuwa Tsh.milioni 106.9
Hivyo
alisema kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wananchi kujiunga na mifuko
ya CHF na NHIF hivyo ni imani yake iwapo uhamasishaji utafanyika
vema kwa mfuko huo wa TIKA pia wananchi wengi watajiunga na
kunufaika zaidi.
Alizitaka
Halmashauri kuwa na mikamkati ya kuboresha huduma ya upatikanaji
wa dawa ,vifaa tiba ,uhusiano mzuri kati ya watoa huduma na
wagonjwa ili asilimia 30 ya Halmashauri ziwe na mikakati na mbinu
endelevu ya uhamasishaji inayoshirikisha jamii kwa ujumla.
Meneja
huyo alisema kuwa fedha za makusanyo yatokanayo na CHF na NHIF
asilimia 2 ya 3 kununua dawa na usimamizi wa upatikanaji na
matumizi ya dawa (CHMT’s)
Post a Comment