Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAMA YAMPA UBALOZI WA HESHIMA MTOTO MMAREKANI

 

  
IMG_7549
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MKE  wa  Rais Mama Salma Kikwete , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA) amemtunuku  Balozi wa kuwatetea  watoto wa kike katika masuala ya elimu kutoka nchini Marekani, Califonia mwenye umri wa miaka (10) Zuriel  Oduwole kuwa  mwanachama (balozi) wa  heshima  wa  taasisi  hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mama Kikwete mara baada ya Zuriel  kuitembelea ofisi  ya WAMA  iliyoko Ikulu jijini Dares Salaam na kufanya mazungumzo  kuhusu  shughuli  inazozifanya .
Mama Kikwete  alimwezea  Zuriel  jinsi taasisi yake inavyofanya  kazi  mbalimbali ikiwemo  ya kuhakikisha watoto  wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata elimu ili waweze kuajiriwa na kujiajiri  ikiwa ni hatua ya kuendeleza maisha yao ya baade na kutimiza ndoto zao.

Kwa mujibu wa  baba wa Zuriel,  Ademola Oduwole alisema mtoto  wake pia  amekuwa akihamasisha wasichana kubadili mtazamo wa  Bara la Afrika  kwa kuwa  huko Marekani watu hawalijuwi bara hilo na wanadhani  ni bara la njaa . 
“Amezindua mradi wa dreaming up dreaming big’ lengo lake ni kuwahamasisha watoto wa kike kuwa na ndoto za kuendelea,” alisema  Oduwole.
 Oduwole   aliongeza kuwa  Zuriel anapenda kuhamasisha kuhusu suala la elimu kwa kuwa ndio njia ya kufikia malengo ya milinea.
 Alisema Zuriel   ameshatembelea nchi  Nigeria,Malawi na Tanzania ambapo alifika Shule ya Msingi ya Olympio na Shule ya Sekondari ya Jangwani na  Shule ya Sekondari  ya wasichana  ya  Marian.Pia ameshafanya mahojiano na marais wanane wa Afrika , ambao ni   wa Tanzania, Mauritius, Kenya,Nigeria, Cape Verde,Sudan ya Kusini na Liberia.
Kwa upande wake Mama   Kikwete alifurahishwa   na juhudi za Zuriel na kumtaka kuendelea kufanya mambo makubwa   katika  kutimiza ndoto zake.
Naye Zuriel   alishukuru kwa ukarimu alioupata kwa Watanzania na ameaihidi kuitangaza Tanzania na WAMA   mahali popote  duniani.
Zuriel alikuwepo nchini kwa kipindi cha siku sita kuanzia jumapili iliyopita  akiwa na  wazazi wake na wadogo zake Azaliah Arielle na Ismachiah,  amerejea Marekani   mwishoni mwa wiki hii.  
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top