
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame
Mbarawa, akikata utepe wakati wa Uzinduzi
wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano ukianzia Shule ya Kambangwa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia
ni Meneja wa Samsung Tanzania Kishor Kumar, wapili ni Mkuu wa kitengo
cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom,
Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,kutoka kushoto ni Mkuu wa
shule hiyo Bi.Theresia Ng’wigulu.


Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa
akimfuatilia mwanafunzi Frank Massay
wa shule ya sekondari ya Kambangwa akitumia komputa zilizounganishwa na
Mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa ushirikiano wa Vodacom na Samsung.
Pamoja nao katika picha (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Huduma za Jamii
cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule,
Mkuu wa shule hiyo Bi.Theresia Ng’wigulu, na Mtaalamu wa komputa wa
Samsung, Julius Giabe.

Waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame,
akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa kitengo
cha Huduma za Jamii cha Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule wakati
wa uzinduzi wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo
wa taifa wa mawasiliano, uliofanyika kwa kuanzia na shule ya Msingi
Kambangwa ya jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kambangwa, wakitoa burudani kwa wageni waalikwa, Wakati wa uzinduzi
wa mpango wa kuunganisha shule za sekondari na Mkongo na Taifa wa Mawasiliano.
---
.Shule za Sekondari nchini kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
·
Kupata komputa na vifaa vya umeme wa jua
Dar es Salaam, Oktoba 22 2013Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amezindua
mpango wa kuziunganisha shule za sekondari nchini na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano huku akitanabaisha
kuwa serikali inathamini na kutambua mchango wa sekta binafsi katika
kuleta maendeleo kwa jamii inayo wazunguka.
Waziri
Mbarawa amesema bila ya kuwa na sekta Rasmi ambayo inatambua mchango
wake kwa jamii inayowazunguka upatikanaji wa maendeleo kwa jamii ya
Watanzania ungeendelea kuwa mgumu, akitolea
mfano mradi huo, Mradi ulioanzishwa na Vodacom na Samsung katika kuunga
mkono mpango wa serikali wa kuunganisha shule za sekondari na mkongo wa
taifa wa mawasiliano.
“Kama
wewe ni mwekezaji au mmiliki wa kampuni binafsi na hautambui matatizo
ya watu wanaokuzunguka sio jambo jema, Ni muhimu sehemu ya faida
unayoipata uwekeze katika kutatua changamoto
zinazowakabili, Tukijenga utamaduni huu tutaweza kuiokoa jamii ya
kitanzania ambayo inahitaji misaada ya aina mbalimbali katika
kujiendeleza” alisema Prof. Mbarawa.
“Kama
ilivyo katika sekta ya Elimu Serikali pekee haiwezi kutatua changamoto
zote zinazoikabili sekta hii, bali tu ni kwa kushirikiana na wadau kama
ilivyofanyika kwa Vodacom na Samsung
kuwezesha mradi wa kuunganisha shule zetu na mkongo wa taifa wa
mawasiliano.
Aidha
Waziri Mbalawa alisema Serikali inunga Mkono harakati za kampuni hizo
katika kuisaidia sekta ya elimu kuendana na kasi ya mabadiliko ya
sayansi na teknolojia.
“Dunia
sasa imepita katika mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia bila
kujenga uwezo na miundombinu katika shule zetu, kwa kutoa vifaa vya
kuwawezesha wanafunzi wetu kujifunza kutokana
na mabadiliko yaliyopo bado elimu yetu haitopiga hatua na jamii ya
Watanzania itaendelea kuwa nyuma siku zite, Serikali inatambua mchango
huu na inaahidi kuwaunga mkono wote ambao wana nia ya dhati ya kuleta
mapinduzi katika elimu.”
Akitoa hotuba yake kwa Waziri Mbarawa,
Mkuu wa kitengo cha Mfuko wa Huduma za jamii, Vodacom Foundation,
Yesaya Mwakifulefule alibainisha kwamba jitihada hizi zinakwenda
sambamba na malengo ya kutoa huduma za kimawasiliano pamoja na kuunga
mkono juhudi za watanzania katika kufikia malengo ya
Mpango wa maendeleo ya Millennia (MDGs).
“Elimu
ndio ufunguo wa maendeleo ya jamii yoyote ile; kwa sababu hiyo Vodacom
inafanya kila jitihada kuhakikisha wanafunzi wanapata nyenzo bora za
kujifunzia bila ugumu wa aina yoyote ile.
Pia katika jamii yoyote ile duniani yapaswa kuzingatia maendeleo ya
kitekinolojia yanayojitokeza, tumekuja kuhakikisha tunawezesha shule
zote nchini zinakuwa na uwezo wa kuyafikia maendeleo hayo.” Alisema
Mwakifulefule na kuongeza.
“Kampuni
yetu imejidhatiti katika kuendelea kuleta mapinduzi katika sekta ya
elimu, Hivi punde tumeanzisha mpango wa kuziwezesha shule zilizoko
maeneo ya karibu na minara ya Vodacom inayotumia
nishati ya jua kuzalisha umeme kupata nishati ya hiyo.” Alisema.
Mwakifulefule
alihitimisha kwa kusema Vodacom Foundation, imewekeza kwa kiasi kikubwa
katika kujenga madarasa na kuyawezesha kwa vifaa mbalimbali, pia
imeziwezesha shule hizo kwa kuzipatia
vifaa mbalimbali vya kujifunzia nchi nzima.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania, Dongha
Jang kampuni yake ina dhamira ya dhati ya kuleta mapinduzi ya elimu
kupitia mradi huu ambao pia unatumia Jenereta
ya umeme jua, (Solar) ambayo itakua ikitoa nishati kwa vifaa vitakavyo
kuwa vinatumika.
“Kwa
kuimarisha nishati ya jua, tunaweza kuzihudumia jamii za kiafrika na
nishati ambayo inapatikana kwa bei rahisi mno, ambayo pia ni rafiki wa
mazingira hivyo kwa kuanzia na shule ya
kambangwa na shule nyingine zitakazo fuata zitanufaika na mradi huu.”
Alisema Jang.
“Samsung
imeamua kuelekeza nguvu zake katika kutatua matatizo ya kielimu lengo
kuu ni kuunga mkono kuendeleza jitihada za viongozi wa Afrika na pia
kupata nguvu kazi iliyoelemika ambayo
ndiyo msingi mkuu wa waajiriwa wa baadae.” Aliongeza Jang.
Kampuni
imehamisha nguvu zake kutoka jitihada za kuwajibika na shughuli
mbalimbali za kijamii na kuunda kitu ambacho kitathaminiwa na jamii kwa
pamoja. Hii ina maana kwamba, shughuli zote
za kielimu, kiafya pamoja na mipango ya kuendeleza jamii itakuwa na
madhumi mawili; ya kuunga mkono kufikia malengo ya kibiashara ya kampuni
na vilevile kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla.


Post a Comment