Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa
Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa COP19/CMP9 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Poland, mjini Warsaw. Rais Kikwete alikuwa anazungumza kwa niaba ya viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika nafasi yake akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).
Rais
Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tokea Januari, mwaka huu,
2013, wakati alipochaguliwa na viongozi wenzake kushika nafasi hiyo
kufuatia kifo cha aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa
Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, Septemba, mwaka jana.
Picha na Ikulu



Post a Comment