Mh:Mwigulu
Nchemba akiwasili eneo la Mkutano Kata ya Mkwiti Wilaya ya Tandahimba
Mkoani Mtwara kwaajili ya Kufungua Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa
Udiwani,Licha ya Mvua Kubwa Kunyesha hadi mwisho wa Mkutano,Wananchi
walikuwa radhi kunyeshewa lakini Wamsubiri Naibu Katibu Mkuu wa Chama
Chao cha CCM ambaye kabla ya Kufika Mkutanoni alikuwa na Ziara ya
Kufungua Matawi ya Chama,Kupokea Wananchama wapya waliojiunga na CCM
Wilaya Ya Tandahimba na kutembelea Mashina ya Chama
Mh:Mwigulu
Nchemba akitoa dakika Moja kwaajili ya Kumuombea Marehemu(aliyekuwa
Diwani wa kata hii ya Mkwiti) ambayo hii loe inafanyiwa Uchaguzi Mdogo
ilikuziba pengo lake Kiutendaji ndani ya chama na Serikali.
Mvua
Kubwa ikiendelea Kunyesha,Naibu katibu Mkuu CCM Bara akiendelea kunadi
Sera za CCM kwa Wakazi wa Kata ya Ikwiti kijiji cha Njia Panda,Mwigulu
Nchemba amewaomba wananchi wa Ikwiti kumchagua Mgombea kwa CCM kwa
sababu CCM imeshaanza kutekeleza Ilani yake ndani ya kata hiyo na Wilaya
yote ya Tandahimba,Wananchi waliomba sana Kupewa Barabara ya Rami Mwaka
2010 wakati wa Kampeni,Rami imeshawekwa kadri ya Maombi yao,Pia soko la
Korosho limeshaimarishwa.
Huyu
alikuwa naye anawania Udiwani,Bahati mbaya kura zake hazikutosha wakati
wa Mchujo lakini ameamua kumuunga mkono MwanaCCM mwenzake,Na sasa Ndiye
meneja kampeni wa Mgombea wa CCM ndani ya Kata ya Mkwiti.
Ameloa
chapachapa Naibu Katibu Mkuu kwa Mvua Kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati
wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni,Lakini Wananchi walikuwa wavumilivu
vya Kutosha na hatimaye kushiriki Mkutano huo hadi dakika za Mwisho kwa
Mapenzi yao Kwa Mgombea na Chama cha Mapinduzi
Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara akimnadi Mgombea wa Udiwani kata ya Mkwiti wa Chama
Cha Mapinduzi Ndugu Nakatanda Arafa Twalib ambaye ni kada Mtiifu wa
Chama Cha Mapindizi kuanzia Ujana wake,
Licha ya
Mvua Kubwa iliyoanza Mapema tu kabla hata Mkutano kaunza,Wananchi
walijitokeza kwa wingi Kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani
Kata ya Mkwiti,Uchaguzi mdogo huu unaofanyika takribani kata 27 Nchi
nzima kutokana na Madiwani waliochaguliwa Mwaka 2010 kwa sababu za Vifo
na Kujuzulu nafasi hizo zimekuwa wazi kwa Muda mrefu na sasa Tume
imeamua Uchaguzi Ufanyike tena.
Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa Mkwiti amewatolea Mfano mmoja
Mwepesi sana "Ukiwa na Touchi yako unahitaji mwanga,Betri ya Kwanza
Umeweka Vizuri(CCM-Rais),Betri ya Pili Umeweka Vizuri (CCM-Mbunge),Betri
ya Mwisho unaweka Gunzi(Upinzani) Itawaka?,HIvyo basi ni Muda Muafaka
Kwa WanaMkwiti Kuendelea kukiunga chama cha Mapinduzi kiendelea kuongoza
ndani ya Kata yao ili maendeleo yatokanayo na Ilani ya CCM yafanyike
kwa Ufanisi.
Kata ya Mkwiti imekuwa Ikiongozwa na CCM tangu k
Post a Comment