Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
WAPINZANI wa Azam FC katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Ferroviario de Beira wamewasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kwanza utakaofanyika Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya Jiji.
Timu hiyo ya Msumbiji imefikia katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Azam Complex kabla ya mechi keshokutwa.
Mchezo huo, utakaoanza Saa 10:00 jioni na kurushwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam, utachezeshwa na marefa kutoka Sudan Kaskazini, chini ya Kamisaa kutoka Somalia, ambao wote wanatarajiwa kuwasili usiku wa leo.

![]() |
| Wamewasili; Ferroviarrio baada ya kutua JNIA leo |
Mapokezi mazuri: Ferroviario wakiwa mbele ya basi la Azam FC liliwapokea JNIA
Azam inacheza kwa mara ya pili mwaka huu michuano hiyo ya Shirikisho, baada ya mwaka jana kutolewa hatua ya 16 Bora na AS FAR Rabat ya Morocco, ikiwa chini ya kocha Muingereza, Stewart John Hall, aliyejiuzulu Novemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog.
Azam imekuwa kambini katika hosteli zake za kisasa zilizopo Azam Complex kwa muda wote wiki hii tangu baada ya mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar Jumapili, ambayo walishinda mabao 4-0 Chamazi.
Viingilio katika mchezo huo vinatarajiwa kuwa Sh. 7, 000 kwa jukwaa la VIP A, Sh. 5,000 VIP B na mzunguko Sh. 2,000.
Mwenendo wa timu ya Azam chini ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon ‘Simba Wasiofungika’ kwa ujumla ni mzuri, hadi sasa ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu kati ya tisa tangu aanze kazi mwezi uliopita.
Azam inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, ni timu pekee inayoendeshwa kisasa nchini ambayo matarajio ni kufuata nyayo za klabu nyingine bora Afrika kama TP Mazembe ya DRC.
Omog alisaini mkataba ma Azam Desemba mwaka jana akitokea klabu ya A.C Leopards ya Kongo Brazavville ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013) na kumaliza ukame wa mataji wa miaka 30.
Aliiachia timu hiyo ubingwa wa Kongo akiwazidi wapinzani wao, Diables Noirs kwa pointi 10 kutokana na kukusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18.
Mwaka juzi (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia.
Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38.
Kadhalika mwaka jana, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.
![]() |
| Kocha mataji; Kocha wa Azam FC, Joseph Marius Omog ataanza kuiongoza timu hiyo katika michuano ya Afrika Jumapili, kujaribu kuendeleza rekodi yake nzuri ya Kongo |
REKODI YA JOSEPH MARIUS OMOG AZAM
Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Kirafiki, Azam Complex)
Azam FC 2-0 Spice Stars (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Tusker FC (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Ashanti United (Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 2-0 Cloves Stars (Robo Fainali, Mapinduzi)
Azam FC 2-3 KCC (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
Azam FC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
Azam FC 4-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bara)

Post a Comment