Kattibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba
zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa katika wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi ambapo nyumba 70 zimekamilika kati ya 90 zitakazojengwa
wilayani hapo.
Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa zinazojengwa katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ngazi baada ya
kukagua mradi wa maji wa Ikorongo,Katibu mkuu ameongozana na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa
Balozi Ali Abeid Karume,mradi huu utakamilika mwezi juni 2014.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza mabomba
kwenye mradi wa maji wa Ikorongo wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpanda
mjini kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili na kuwapongeza kuwa
wachapakazi hodari katika kusimamia maendeleo yao na kuwataka kuwa
makini na wanasiasa kwani mwisho wa siku hoja zao haziwasaidii wao
kwenye maisha yao ya kila siku.
Katibu
wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa baada ya kumaliza
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili wilayani
Mpanda.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina
namba 32 Makanyagio Mpanda na kuwasihi wakazi hao kuchagua viongozi
sahihi na wenye sifa za kuwaongoza.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa shina namba
32 Makanyagio wilaya ya Mpanda walipomtembelea Balozi wa Shina Ndugu
Tobias Kazimzuri.
Post a Comment