PAZIA
la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 linafungwa kesho
aprili 19 kwa timu zote 14 kushuka uwanjani katika miji tofauti nchini.
Ligi inamalizika kesho wakati timu tatu zimeshajihakikishia nafasi tatu za juu.
Azam fc wametwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote.
Yanga wamechukua nafasi ya pili wakiwa na pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote chini yake.
Mbeya City nao wameshika nafasi ya tatu kwa pointi 46 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya chini yake.
Simba sc wao wao wapo mbioni kuisaka nafasi ya nne kwa pointi zao 37 baada ya kucheza mechi 25.
Nafasi
ya tano wapo Kagera Sugar wenye pointi 35, na endapo Simba watafungwa
kesho na wao wakashinda, basi Mnyama anaweza kumaliza ligi katika nafasi
ya tano.
Katika mechi zote 7 hapo kesho, mechi tatu pekee zina hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka nchini.
Mechi
ya kwanza iliyovuta hisia za mashabiki wa soka ni ile ya Yanga dhidi ya
Simba sc ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Timu
hizi zitakutana zikiwa na mafanikio tofauti msimu huu ambapo Yanga
wameambulia nafasi ya pili, huku Mnyama akijikongoja katika nafasi ya
nne.
Simba na Yanga zinakutana jumamosi, huku Yanga wakiwazidi wenzao kwa mafanikio msimu huu.
Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar Es Salaam
0712461976
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
Post a Comment