Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA toka Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.
Emmanuel Mahinga akitoa maelezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam (hawapo pichani) kuhusu jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za
Umma (EPICOR 9.05) unavyofanya kazi na malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huo ikiwemo kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.
Afisa
Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Elisa Rwamiago (katikati)akifafanua
kwa waaandishi wa habari jinsi Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma
(EPICOR 9.) utakavyoongeza tija katika utendaji wa Serikali za Mitaa na
kuondoa malalamiko ya kuwepo mianya ya vitendo vya ubadhilifu wa fedha
za umma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi
Rebecca Kwandu.kulia, ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi
Georgina Misama
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi Rebecca Kwandu (kushoto)
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam
kuhusu faida za matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR
9.05) Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Halmashauri 133 na
Mkoa 21 ya Tanzania Bara imeunganishawa katika mfumo huo, katikatika ni
Afisa Msimamizi wa Fedha (TEHAMA) toka TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama. (FS)
Post a Comment