Mkurugenzi
wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja toka Bohari ya Dawa (MSD)
Bw. Edward Terry Kulia akizungumza na waandishi wa habari leo katika
ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya mpango wa bohari hiyo kupanua
maghala ya kuhifadhi Dawa na Vifaa tiba kama moja ya hatua za
kuboresha huduma zinazotolewa na Bohari hiyo . Kushoto ni Mkurugenzi wa
Manunuzi wa Bohari hiyo Bw. Heri Mchunga.
*******
Na Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yajipanga kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa uhakikika katika hosipitali zote za umma hapa nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja wa
Bohari ya dawa (MSD) Bw.Edward Terry wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza
Terry amesema kwa hivi sasa Bohari ya Dawa imejipanga vizuri
kuhakikisha kuwa dawa zinafika kwa wakati katika maeneo yote
zinakohitajika kwa kuweka mfumo mzuri unahakikisha kuwa dawa zikifika
zinatumika kwa wananchi waliokusudiwa .
Akieleza
Zaidi Terry alisema kuwa mnamo mwaka 2010 walifanya majaribio ya
utaratibu wa kupeleka dawa moja kwa moja kwenye vituo vya afya ambapo
utaratibu huu umeonyesha mafanikio makubwa hivyo ni imani ya Bohari ya
Dawa kuwa utaratibu huo utasaidia sana kuondoa tatizo la upatikanaji wa
dawa hasa maeneo ya vijijini.
Kwa
upande wa Kudhibiti upotevu wa dawa katika vituo vya Afya na Hosipitali
Terry amesema dawa zinazotolewa na Serikali zitakuwa na alama maalum ya
kuzitofautisha na zile zinazouzwa katika maduka binafsi ili kuondoa
tatizo la wizi wa dawa zinazosambazwa na Bohari ya Dawa hapa nchini.
Kuhusu
Faida za kuweka alama maalum katika dawa za Serikali Terry amesema
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu
upatikanaji wa dawa mara wanapahitaji huduma hiyo katika hosipitali au
vituo vya afya kwa kuwa tatizo la wizi litakoma.
Kwa
wale watakaobainika kujihuisisha na wizi wa dawa za Serikali ,Terry
amesema hatua kali zitachukuliwa bila kuwaonea haya na kutoa wito kwa
wananchi kuwafichua wale wote wanaojihusisha na wizo huo ili mkondo wa
sheria uchukue nafasi yake.
Bohari
kuu ya Dawa imefungua kituo cha Kusambaza Dawa cha Muleba ,Mkoani
Kagera kitakachosaidia kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Geita na Kagera
kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu.


Post a Comment