Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ALI KIBA Afunguka baada ya kuwa kimya kwa miaka 3


KIBA Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki Ally Salehe Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa kando ya muziki kwa muda mrefu.
Alikiba ambaye aliachia wimbo wake wa mwisho “My Everything” Novemba 2012 hajawahi kuachia tena wimbo mwingine, licha ya kutoa kazi kadhaa alizokuwa akishirikishwa na mdogo wake msanii Abdu Kiba ukiwamo “Kidela”.
Starehe ilikaa kitako na msanii huyu aliyewahi kutamba na wimbo wake wa kwanza “Sinderela” mwaka 2007, nyumbani kwake Kunduchi Beach na ambapo aliainisha mambo makubwa matatu yaliyomfanya asimame kwa muda kuachia kazi za muziki.
“Kuna mambo matatu ya msingi niliyokuwa nayafanya kwa kipindi hiki cha miaka mitatu. Awali ya yote niliamua kusimama ili kumlea mwanangu, malezi ya mtoto yalinifanya niegemee huko hadi umri wake usogee ndipo nirudi kwenye muziki,” anasema pasipo kufafanua vizuri iwapo ni wa kike au wa kiume.
Anasema familia yake ni kitu chenye uthamani mkubwa kwake ndiyo maana alijitoa ili kuhakikisha inakaa sawa.
       
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top