Wakati
Serikali ikihaha kusaka fedha za kugharimia miradi ya maendeleo kwa
mwaka ujao wa fedha, kumekuwa na shaka kuhusu uhalisia wa hesabu za
matumizi zilizotengwa kwa ajili ya Ofisi ya Hazina.
Ofisi
hiyo chini ya Fungu 21 imeomba kuidhinishiwa kiasi cha Sh790,325,216,000
kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kupitia katika idara
zake kati ya hizo zaidi ya Sh50 bilioni zikiwa ni kwa ajili ya safari na
posho mbalimbali.
Itakumbukwa
kuwa tangu kumalizika kwa uwasilishaji wa bajeti za kisekta kupitia
wizara za Serikali, Kamati ya Bunge ya Bajeti imekuwa katika mashauriano
na Serikali, kusaka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa baadhi ya miradi
ya maendeleo ambayo ilionekana kuwa ni muhimu.
Katika
mashauriano hayo, Serikali na kamati zilikubaliana kukata asilimia nane
ya fedha za matumizi mengine katika kila wizara na kuchukua kiasi cha
Sh2 bilioni kutoka Hazina maalumu ya Serikali ili kupata Sh225.281
bilioni kwa ajili ya maeneo yaliyokuwa na upungufu.
Wakati
hayo yakiendelea mabilioni ya fedha yametengwa kwa ajili ya kazi za
idara zilizopo chini ya Hazina ambazo kimsingi zinapaswa kufanywa na
watumishi wa Serikali katika kazi zao za kawaida bila kupewa malipo ya
ziada.(P.T)
Ufafanuzi
wa matumizi ya fedha uliotolewa kwenye Randama za Hazina unaonyesha
kuwa baadhi ya fedha zimetengwa kwa jumla tu, pasipo kuonyesha uhalisia
wa matumizi yake.
Miongoni
mwa maeneo yaliyotengewa kiasi kikubwa cha fedha ni kile kinachoitwa
malipo ya tuzo kwa watumishi, vifaa vya nyumbani kwa baadhi ya
wakurugenzi na wakuu wa idara, posho za vikao maalumu na malipo kwa
ajili ya kazi ambazo kimsingi ni wajibu wa idara husika.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina,
alisema Serikali haijapunguza matumizi mengineyo katika bajeti zake za
mwaka wa fedha 2014/2015 kama ilivyoahidi katika bajeti iliyopita.
Mpina
ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa (CCM), alisema Serikali iliahidi
kupunguza matumizi mengineyo (OC) kwa kiasi cha Sh283 bilioni katika
mwaka wa fedha 2013/2014, lakini hakuna ushahidi kwamba imetekelezwa.
"Ahadi
hiyo ilitolewa kwa maandishi na Waziri wa Fedha, lakini hadi mwaka mwaka
huu wa fedha unaelekea mwisho hakuna mchanganuo wowote unaoonyesha
kupunguzwa kwa matumizi hayo," alisema Mpina na kuongeza: "Bunge
lilihakikishiwa kuwa kuhamishwa kwa fedha hizi na kupelekwa katika
miradi ya maendeleo hakutaathiri utendaji wa Serikali. Lakini cha
kushangaza, bajeti iliyowasilishwa matumizi mengineyo (OC)
yameongezeka."
Alisema
wakati wa uwasilishaji wa maoni ya kamati yake kuhusu Bajeti ya Wizara
ya Fedha kwa mwaka 2014/2015, kamati ilihoji kwa nini kwa kipindi kirefu
Serikali imeendelea kutetea matumizi ya aina hii kuwa ni muhimu, lakini
Serikali haijawahi kuleta mchanganuo wa matumizi hayo (matrix) ili
kuthibitisha umuhimu unaosisitizwa?
Idara ya Bajeti
Post a Comment