Cecilia Hamis (kulia) akiwa na mume wake (mtuhumiwa) Hamis Juma.
LILE sakata
la mume aliyetajwa kwa jina la Hamis Juma (pichani akiwa na mkewe),
mkazi wa Majohe Mji Mpya, Ilala jijini Dar kudaiwa na mkewe, Cecilia
Hamis kwamba amempa mimba mbwa yameibuka mapya, limeyanyaka.
Ijumaa iliyopita, tulifika kwenye ofisi
za Taasisi ya Kutetea Haki za Wanyama ambapo mmoja wa maofisa aliyedai
si msemaji maalum, alisema wapo katika mchakato wa kufuatilia madai ya
mke wa mtuhumiwa huyo kisha kumpandisha mahakamani kujibu mashitaka ya
kumdhalilisha mnyama huyo.
“Sisi ishu yetu si kufuatilia kama kweli
amempa mimba bali ni kujiridhisha kama kweli yule mzee ametembea na
mbwa hilo linatosha kabisa kumfikisha kortini,” alisema afisa huyo na
kuomba jina lake lisitajwe.
WAGOMA MBWA KUUAWA
Jingine jipya lililotua linadai kuwa,
baadhi ya majirani wa nyumbani kwa Hamis wamegoma mbwa huyo kuuawa baada
ya wengine kutaka kufanya hivyo wakisema hali hiyo itaweza kusababisha
mdaiwa huyo kufanya matukio mengine nje ya nyumba yake.
MENGINE TENA
Katika hatua nyingine, limebaini kuwa,
kumbe mwanaume huyo ana sakata lingine ambapo ana kesi kwenye Mahakama
ya Mwanzo Ukonga jijini Dar akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia fujo
jirani yake.
Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama,
ilidaiwa kuwa Hamis alifika nyumbani kwa Alanus Haule ambaye ni jirani
yake saa saba usiku wa siku ya tukio akiwa na silaha za kienyeji na
chepe akiwa amelewa na kuanza kumtolea maneno ya vitisho huku akijua ni
kosa kisheria chini ya kifungu cha sheria 89 (1) B CAP 16.
Kesi hiyo yenye No 873/2014 ambayo
inasikilizwa na Hakimu Mwandamizi, Raia Omary kwa mara ya mwisho
ilisikilizwa Julai 3, mwaka huu na kuahirishwa hadi Septemba 11, mwaka
huu na yuko nje kwa dhamana.
Habari hii kuhusu Hamis Juma kudaiwa kumpa mimba mbwa, kwa mara ya kwanza ilitoka >>HAPA<< Agosti 5-11, 2014 ambapo kichwa cha habari kilisomeka ‘MUME WANGU KAMPA MIMBA MBWA.’
on Wednesday, August 13, 2014
Post a Comment