Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LADY JAYDEE SASA AHAMIA HOTELINI!


 Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’.
********
 NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu. 


Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005. 

Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani  hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake. 
Hata hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa  iliyopita lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli. 

Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani.


Judith Wambura ‘Jide’ akipozi.

 Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!


Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka nayo. 

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki.“Ni kweli Anaconda (Jide) anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo,” alisema mtu huyo.

Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi.
Imeandikwa na Shakoor Jongo, Gladness Mallya na Chande Abdallah.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top