Jeneza la Mwili wa Marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo likiteremshwa makaburini kwa ajili ya mazishi.
Mchungaji akiendesha ibada ya mazishi ya Marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo
Waomboleaji wakiuzika mwili wa marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo
Mmoja wa Mbwa wanaodaiwa kumuua marehemu Iblahim Faraja Chipungahelo ameuwawa.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Bazil Makungu Ludewa
MWANAFUNZI
wa shule ya msingi Ludewa mjini katika mkoa wa Njombe Iblahim Faraja
Chipungahelo ameuawa na kisha kuliwa nyama na mbwa wanaosadikika kuugua
kichaa kwa kukosa chakula kwa muda mrefu.
Tukio
hilo la kusikitisha na lililoleta simanzi kubwa kwa wakazi wa Ludewa
mjini lilitokea August 8 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo
la Ikulu ambapo marehemu Chipungahelo pamoja na wenzake walikuwa
wakipita njia karibu na nyumba ya mtu aliyejulikana na kwa jina la Bosco
Lingalangala kwenda kuchuma mapera kama ilivyo destuli yao.
Mashuhuda
wa tukio hilo mama Kumba na mama Haule wakazi wa kitongoji cha Ibani
katika kata ya Ludewa kwa pamoja walieleza kuwa wakiwa nyumba walisikia
kelele za watoto jirani huku wakimwita mwenzao marehemu bila mafanikio.
‘’’’ Tulipowauliza
walisema kuwa mwenzao Ibrahim amekamatwa na mbwa na ndipo
tulipokusanyika na kwenda kumwokoa mtoto lakini tulipofika eneo la tukio
tulimkuta mbwa wakiendelea kumla marehemu huku amelala kifudifudi
lakini tulishindwa kumwokoa na ndipo tukakimbia kutoa taarifa kituo cha
polisi.””” walisema akina mama hao kwa uchungu
Kwa
mujibu wa taarifa ya daktari Sira Rajabu wa Hospitali ya wilaya ya
Ludewa aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu alisema mtoto Ibrahim
alikuwa na majeraha makubwa mwili mzima huku paja la mguu wake wa kulia
likiwa limeliwa na kuondolewa nyama.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi
Fulgensi Ngonyani alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watu mbalimbali akiwemo
mmiliki wa mbwa hao ambaye inasadikika kuwa ananishi jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
na mwandishi wetu mganga wa mifugo Simoni Haule alisema kuwa mbwa hao
wa bwana Bosco Lingalangala hawajapata chanjo zaidi ya miaka miwili sasa
kwa hiyo tayari mbwa hao wanaugua ugonjwa wa kichaa ambacho hawawezi
kupona tena na dawa iliyobaki ni kuuawa tu.
Mmiliki wa mbwa hao Bosco lingalangala hakupatikana ili kuzungumzia suala hilo kwa sababu simu yake ya mkononi haikupatikana.
Hata
hivyo akiwa makaburini diwani wa Kata ya Ludewa Monica Mchiro
aliwaambia na kuwatahadharisha waombolezaji na wananchi waliohudhuria
mazishi kuwa mawasiliano yamefanywa kati yake na mmiliki wa mbwa hao
lakini majibu aliyoyatoa hayana ushirikiano kwa sababu ameahidi kuchukua
hatua za kisheria kwa yeyote atakaye husika kuwadhuru mbwa wake.
Hata
hivyo habari kutoka kwa majirani ambao hawakupenda kutaja majina yao
walisema mbwa hao hufungiwa kwenye banda na hupewa nyama mbichi kwa
kurushiwa na wahudumu lakini siku hiyo walifunguliwa na kuanza kuzagaa
kwa nia ya kujitafutia chakula wenyewe baada ya kukosa kwa muda mrefu.
Post a Comment