Rasmi: Thomas Vermaelen ametua Barcelona baada ya Asrenal kugoma kuwauzia silaha Man United
NAHODHA
wa Arsenal, Thomas Vermaelen amejiunga na Barcelona kwa dau la Pauni
Milioni 15 baada ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London kugoma kuwauzia
silaha wapinzani wa Ligi Kuu England, Manchester United.
Beki
huyo Mbelgiji amesaini Mkataba wa miaka mitano na vigogo hao wa
Hispania, ambao unaaminika utamfanya awe analipwa Pauni 80,000 kwa wiki.
Vermaelen
amekuwa Arsenal kwa miaka mitano na miaka miwili akiwa Nahodha wa
kikosi cha Arsene Wenger, lakini msimu uliopita alijikuta anawekwa
benchi Laurent Koscielny na Per Mertesacker.
Post a Comment