Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto Bw. Marcel Katemba akiongea na waandishi wa habari(
Hawapo pichani)kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuyajengea mazingira
mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki
na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo katika jamii, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo
Jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo
Bw. Erasto Ching’oro.
Na Jovina Bujulu-MAELEZO.
Serikali
kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imeendelea
kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kushiriki
kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam.
Mercel
alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo ikiwemo
utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 na
Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 na marekebisho yake
ya mwaka 2005.
“Sera
hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo kushiriki
kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na
ushirikano” Alisema Marcel.
Marcel
aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea kusimamia
sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya uratibu
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa
sekta hiyo.
Aidha
Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za maadili
ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala, kutandaa na kuboresha
huduma zinazotolewa na mashirika hayo.
Akifafanua
zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s umeimarika
kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau mbalimbali wa
mashirika yasiyo yakiserikali.
Pia
Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo ikiwa
ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
Juhudi
za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa wananchi
kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya wananchi 35,000
ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679 kote nchini.
Post a Comment