Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Sophia
Simba akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu
maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya
Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
|
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni
mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akichangia mada leo
mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika
Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3
Septemba, 2014.
|
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Angellah Kairuki akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake
kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu
ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba,
2014.
|
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa akitoa neno la shukurani mara baada ya kumalizika kwa utoaji
mada kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu
ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge
Wanawake uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
|
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt.
Angelina Samike akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake
kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Felister Bura akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake
kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba,
2014.
|
Mhadhiri Msaidizi wa Sheria katika Chuo Kikuu
cha Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge
Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu
ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba,
2014.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
wakifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na baadhi ya
wajumbe wa bunge hilo leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa
waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa
uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
|
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara (kulia)
akisalimiana na mjumbe mwenzie wa Bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki mara baada
ya kumalizika kwa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa (kulia) akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzie wa bunge hilo,
Mhe. Martha Mlata mara baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake uliofanyika
mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma
---- Na Benedict Liwenga, Dodoma.
UMOJA wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG)
wamejipongeza kwa hatua kubwa waliyofikia na manufaa waliyoyapata wanawake
katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Wabunge
hao ambao pia ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakati walipofanya semina
iliyoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao kuhusu maandiko ya kisheria na manufaa
waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Akitoa mada wakati wa Semina hiyo, Katibu Mkuu
wa TWPG ambaye pia ni Mjumbe wa bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa
moja ya manufaa ambayo wanawake watayapata katika Katiba mpya ijayo ni kuhusu
masuala ya uongozi ulio bora wenye kuzingatia sifa na weledi katika michakato
ya ajira na uteuzi ambapo suala hilo limetiliwa nguvu katika Ibara ya 208,
Ibara ndogo ya kwanza kipengele C ambapo katika masuala ya uteuzi na mambo ya
ajira katika nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Umma utazingatia uwezo wa
kitaaluma, weledi, ujuzi, usawa wa jinsia hivyo suala la usawa wa jinsia
limezingatiwa.
Mhe. Kairuki ameongeza kuwa, katika Sura ya Kumi
inayohusu masuala ya Bunge kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 129 ibara ndogo ya
Nne, amesema kuwa kwa kutambua kuwa Bunge ndiyo mhimili muhimu wa dola, Katiba
inayopendekezwa imekusudia kurekebisha kasoro iliyopo ya uwakilishi mdogo wa
wanawake bungeni ambapo hivi sasa kuna asilimia 36.6% ya wanawake bungeni.
“Kupitia Katiba hii inayopendekezwa kupitia
Ibara ya 129 Ibara ndogo ya Nne tutakuwa na uwakilishi uliosawa baina ya
Wabunge wanawake na Wabunge wanaume”, alisema Mhe. Kairuki.
Aidha, alieleza kuwa katika Sura ya 12 inayohusu
Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama
imepewa wajibu katika ajira mbalimbali na uteuzi kuhakikisha kuwa inazingatia
usawa wa jinsia.
Naye Mhadhiri Msaidizi wa Sheria kutoka Chuo
Kikuu cha Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe amewapongeza wajumbe hao wanawake kwa
kazi kubwa walioifanya katika kudai haki zao huku akizungumzia juu ya baadhi ya
Mikataba ambayo Tanzania imeridhia pamoja na baadhi ya itifaki za Kimataifa
yakiwemo maazimio mbalimbali ambayo Tanzania kama Mwanachama wa Jumuiya ya
Kimataifa imeridhia na hatua kubwa iliyopiga.
Mpelumbe amesema kuwa katika Azimio la 1948 (Universal Declaration of Human Rights) katika
Ibara yake ya kwanza inaelezea juu ya mambo ya usawa kati ya mwanamke na
mwanaume, lakini pia suala la usawa kati ya binadamu wote umepewa kipaumbele.
Mpelumbe ameongeza kuwa licha ya Mikataba ya
Kimataifa pamoja na sheria mama zilizopo sasa nchini, haki za wanawake
zinatakiwa kujengewa ulingo wa kuzisemea mara kwa mara ili watu wapate
kuzielewa vizuri.
“Nchi za wenzetu wameweka jitihada za dhati
kabisa katika kujenga uwezo wa mwanamke na jitihada hizi zinatokana na utiaji
sahihi na kuridhia hii Mikataba ya Kimataifa mbalimbali ambayo inatoa haki za
wanawake lakini hatua ya pili ni kwa kuchukua hatua za msingi za kikatiba na
kisheria kuziweka hizo haki za mwanamke katika ulingo wa Kimataifa zionekane
zaidi na kwa uwazi kabisa katika Katiba ya nchi na Sheria za nchi”, alisema
Mpelumbe.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni
mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro amesema kuwa mshikamano ambao
Wabunge wanawake wa Bunge hilo wameuonyesha ni mkubwa sana kwani wameweza
kushikamana bila ya kujali Vyama walivyotoka, Kundi waliloliwakilisha , Sura na
hata afya zao.
Dkt. Migiro ameeleza kuwa suala la hamsini kwa
hamsini limekaa vema katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa na
itawapa wanawake wengi msingi wa kuteremka chini kwani wanawake wengi
wamejitokeza kwa wingi katika Mabaraza ya Kata na Taasisi zenye mrengo
unaofanana na wamekuwa waaminifu ndani ya Bunge Maalum.
“Katiba hii ni yenu, tutakwenda kuipigia debe
kwani ni Katiba ambayo imetuweka mahali pazuri kuimarisha haki ndani ya nchi
yetu, maslahi ndani ya taifa letu, kuimarisha Muungano wetu na umoja wetu”,
alisema Dkt. Migiro.
|


Post a Comment