Kuanzia
leo longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa
historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa mchana
kweupe.
- Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
- Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
- Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
- Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
- Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
Kuanzia
jana huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa ikionyesha tick
mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma
kubainisha kuwa umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.



Post a Comment