Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Chadema wachuana ubunge Tabora Mjini


WANACHAMA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametangaza kuingia katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa katika Ukawa kuwania ubunge jimbo la Tabora Mjini.
 
Walitambulishwa jana katika mwendelezo wa mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na uongozi wa chama hicho mkoa ambao jana ulifanyika katika kata ya Mpera katika Manispaa ya Tabora.
 
Wanachama wanaowania kuteuliwa na chama hicho ni Profesa Hamba Makambi, Raymond Maganga, Said Mwakasekela, Furaha Kisanji na Peter Mkufya.
 
Mwanachama mwingine, Rehema Raphael anawania viti maalumu wanawake. Wagombea hao wa chama hicho watachujwa Julai 25 na kubaki mmoja atakayepambanishwa na mwingine kutoka kila chama kinachounda ukawa kabla ya kupatikana mgombea atakayepeperusha bendera ya ukawa kwenye jimbo la Tabora Mjini linaloongozwa na Ismail Rage wa CCM.
 
Mratibu wa Kanda wa Chadema, Christopher Nyamwanji alisema viongozi wasiokuwa na dhamira ya kuwakomboa watanzania ndio wameifikisha nchi pabaya.
 
Alieleza kuwa pamoja na mkoa kuwa na misitu katika maeneo mengi, inashangaza kuona wanafunzi wakikaa chini madarasani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top